Jumamosi, 13 Desemba 2014

CAG akague Bodi ya Sukari- Waziri Chiza

  Dar es Salaam, Serikali imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kukagua Bodi ya Sukari ili kubaini kama kuna aliyehusika kutoa kibali cha kuagiza sukari kutoka nje kwa mwaka 2013/14. Kauli ya Serikali imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Zitto Kabwe kusema kuwa ataanza...

Karatasi za kupigia kura zanaswa D’Salaam

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika kesho nchini kote. Picha na Venance Nestory .  Na Ibrahim Yamola na Kelvin Matandiko, Mwananchi Dar es Salaam. Wakati Uchaguzi wa Serikali...

Al-Bashir Asema Ameishinda ICC

Rais Omar al-Bashir wa Sudan amedai ushindi katika mvutano wake na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, baada ya mkuu wa mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, kusimamisha uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu wa vitani katika jimbo la Darfur. Rais Bashir, ambaye alishtakiwa kwa mauaji ya kikabila mwaka wa 2009, alisema ICC imeshindwa katika kile alichoeleza kuwa juhudi za ICC za kuiaibisha Sudan. Alisema wananchi wameamua kuwa afisa yoyote wa Sudan...

Mahujaji Milioni 17 Wakusanyika Karbala

Mamilioni ya mahujaji wa Kishia wamemiminika katika mji wa Karbala, Iraq, kwa ibada ya kila mwaka ya Arbaeen ingawa kuna tishio la mashambulio ya wapiganaji wa madhehebu ya Sunni wa Islamic State. Wakuu wa Iraq wanasema mahujaji zaidi ya milioni 17 wamekusanyika Karbala kuhudhuria Arbaeen. Picha zilizopigwa kutoka angani zinaonesha barabara zinazoelekea Karbala kama mito ya watu waliovaa nguo nyeusi, hadi upeo wa macho. Na kuna wasiwasi...

Maelfu Waandamana Washington na New York

Maelfu ya watu waandamana leo katika bara-bara za miji ya Washington na New York kupinga mauaji ya wanaume weusi wasiokuwa na silaha yaliyofanywa na polisi wa Marekani, ili kulitaka bunge lilinde wananchi. Taarifa iliyotolewa na kiongozi wa kutetea haki za raia, Al Sharpton, ilieleza kuwa bunge linahitaji kuchukua hatua kubadilisha sheria na hali bara-barani. Kati...

Hafla ya kukabidhi Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Mhe Stephen Masele (aliyesimama katikati na pama) akishuhudia halfa fupi ya kusaini makabidhiano ya eneo la Mgodi wa Resolute kwa Chuo cha Madini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha  Madini Dodoma, Mjiolojia Mwandamizi Subian Chiragwile, katikati ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally...

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PIL,ALHAJ MWINYI ATEMBELEA MIRADI MBALIMBALI YA NSSF JIJINI DAR LEO

Rais Mstaafu wa awamu ya pili nchini Tanzania,Alhaj Ali Hassan Mwinyi ametembelea miradi mbalimbali ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo aliweza kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni, daraja ambalo linategemea kukamilika mwezi wa saba mwaka 2015 na vilevile amepata nafasi ya kutembelea Ujenzi wa nyumba za shirika...