Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN
CITY Bw. Hasan Rizvi akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani)
mashine za michezo mbali mbali itakayotolewa kipindi cha sikukuu ya
Pasaka wakati wa mkutano alioufanya katika eneo la Fun City Kigamboni
jijini Dar es Salaam. Pia aliongeza kuwa kwa sasa kampuni yake
imeeongeza mitambo yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita
tofauti kwenye bwawa kubwa la kuogelea.
Mitambo
ya kisasa iliyofungwa katika eneo la Fun City ambayo itawawezesha
wananchi kupata burudani kabambe zenye ubora wa kimataifa kwani hakuna
mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo.
Mawimbi yanayotengenezwa kwa mitambo ya kisasa katika bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fun City,
Moja ya Bwawa la kuongelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi akionyesha vigari vya mchezo.
Bembea za kutosha.
Bembea za watoto.
Mapokezi ya Fun City.
Eneo la Fun City linasehemu ya Ibada.
Sehemu ya huduma ya kwanza nayo inapatikana hapa.
Sehemu ya moja ya sehemu ya bembea za magari ikiongesha madhari nzuri za kiota cha burudani cha Fun City.
Vigari vya umeme vinavyopita ndani ya maji.
Wakati
Watanzania wakiwa kwenye maandalizi ya sikukuu ya Pasaka kampuni ya
Green Stars Industry inayomiliki eneo la FAN CITY limeongeza mitambo
yenye uwezo wa kutengeneza mawimbi ya aina sita tofauti kwenye bwawa
kubwa la kuogelea.
Mtambo huo wa aina yake utaongeza hamasa kwa waogeleaji kuhisi kama wapo baharini.
Akizungumzia
mtambo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Fan City, Bw. Hasan Rizvi amesema,
lengo la kuoberesha michezo hiyo ni kuwawezesha watanzania kufurahia
michezo hiyo pamoja na familia zao wakati huu wa Pasaka.
Ameongeza
kuwa mitambo ya kisasa iliyofungwa katika eneo lake itawawezesha
wananchi kupata burudani kabambe yenye ubora wa kimataifa kwani hakuna
mahali popote Afrika Mashariki mitambo hiyo inapatikana.
“Tumefunga
mtambo huu ambao utakua ukitengeneza mawimbi ya aina sita tofauti
kwenye bwawa kubwa la kuogelea lililopo hapa Fan City, lengo letu
nikutoa burudani zaidi kwa watu wanaotembelea hapa”.Alisema Rizvi.
“Tumefanya
uwekezaji wa mashine za kisasa za michezo mbalimbali kwenye eneo letu
ili kutoa burudani nzuri na za kipekee kwa wananchi wanaotembelea eneo
hili na hasa wakati huu wa Pasaka”. Alisisitiza Rizvi. Fan City iliyopo
Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Fun
City imekuwa ikitoa burudani safi ya michezo mbalimbali kwa familia na
katika kipindi hiki cha Pasaka imeandaa michezo kama Sarakasi,
Mazingaombwe na zawadi kemkem kwa watakaotembelea eneo hilo. Picha zote
na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog
0 maoni:
Chapisha Maoni