Jumamosi, 31 Mei 2014
Ijumaa, 30 Mei 2014
MAJIBU YA ZITTO BAADA YA KUHUSISHWA KUWANYONYA WASANII WA KIGOMA ALL STARS.
Unknown 07:09
Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.
Leo tarehe 29 Mei, 2014 Msemaji wa
Kambi ya Upinzani kuhusu Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni
amenituhumu kuhusika na kinachoitwa ufisadi katika Shirika la TANAPA na
NSSF.
Nasikitika kwamba katika hali niliyonayo ya kumwuguza mama yangu
naingizwa kwenye siasa za majitaka. Kwa sasa nitatoa maelezo kwa ufupi
ili kuondoa upotoshaji.
Kampuni ya LekaDutigite inamilikiwa na wasanii 15 ambapo kila mmoja
ana hisa 5% ambazo niliwalipia ili waweze kushirikiana katika kazi zao.
Hisa 25% zilizobakia zinamilikiwa na kampuni ya Gombe Advisors ambayo ni
kampuni isiyofanya faida (Company limited by guarantee) na haina
maslahi yeyote ya kibiashara (not for profit company). Hivyo Mimi
binafsi sina maslahi yeyote ya kifedha zaidi ya kuwasaidia wasanii hawa
katika kazi zao mbalimbali.
Wasanii wa Kigoma AllStars wamefanya kazi na TANAPA na NSSF, kazi
ambazo zinajulikana na zipo. Kwa upande wa TANAPA wasanii hawa waliandaa
kazi ya kuitangaza Hifadhi ya Saadani na walilipwa. Kwa upande wa NSSF
wasanii hao walitunga wimbo na video yake (http://m.youtube.com/watch?v=sMl8T-RkIdM ) na wimbo huo unatumika katika Shirika hilo.
Vile vile walifanya matamasha mbalimbali ya kuhamasisha watu kujiunga
na NSSF. Wasanii wa Kigoma All Stars wote ni wanachama wa Mfuko huo.
Katika kazi zote hizi Mimi binafsi sijafaidika kwa namna yeyote ile
kifedha. Kauli yeyote ya kujaribu kuonyesha kazi hizi za wasanii ni
ufisadi ni kauli za kusikitisha na kukatisha tamaa kwa mtu ambaye
anajaribu kusaidia wasanii kufaidika na kazi zao za sanaa.
Toka mwaka 2012 nilipoanza kujitokeza kusemea wasanii watu kadhaa
wenye maslahi na tasnia hii wamekuwa wakinikatisha tamaa na hata wengine
kuona nimewaingilia kazi zao.
Hivi sasa wasanii wa Kigoma AllStars ni wanahisa katika kampuni ya
PERA Africa limited ili kufaidika na biashara ya miito ya simu. Yote
haya nilifanya kwa uchungu nilionao kwa vijana wetu na sio kwa kutaka
kufaidika kifedha. Nimeumizwa sana na tuhuma hizi za kuokoteza okoteza.
Inaniumiza zaidi kutokana na ukweli kwamba ninamwuguza mama yangu
mzazi, kipindi ninachohitaji kutiwa moyo na kuombewa hata na maadui
zangu kisiasa. Kipindi ambacho mama yangu yupo mahututi, tena mjumbe wa
kamati kuu ya chama ambacho watoa tuhuma wanatoka, pole ninayopewa ndio
hiyo. Hakuna namna ya kukosa ubinaadamu zaidi ya hivi.
Najua wajibu wangu ni kusimamia Mashirika ya Umma na nikiwa mpigania
uwajibikaji nipo makini sana kuhakikisha sina mgongano wa maslahi katika
mambo yangu. Ndio maana sina biashara yeyote ile ili kuhakikisha
natimiza wajibu wangu kwa uadilifu mkubwa. Napata 'moral authority' ya
kutaka uwajibikaji kwa sababu nafanya kazi zangu kwa misingi hiyo 'at
arms length'.
Hivyo ninataka mara moja CAG afanye ukaguzi wa kazi za wasanii hao
kwenye NSSF na TANAPA. Pia achunguze kama Gombe Advisors ( company
limited by guarantee) ina maslahi yeyote ya kifedha katika kazi hizo za
wasanii. Nataka pia Shirika la NSSF na TANAPA waweke wazi mchakato wa
kazi zao na wasanii hawa kupitia LEKADUTIGITE Limited.
Zitto Kabwe
Mei 29, 2014
Dar Es Salaam
Picha za mume wa msanii Recho, George Saguda akiwa na simanzi baada ya kumpoteza mkewe na mtoto
Unknown 07:01
Mume wa marehemu Recho, George Saguda,akiwa na simanzi nzito kufuatia kifo cha mkewe na mtoto.
Baadhi ya wasanii wa Bongo
Movies wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya taarifa za
msiba wa msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho'
Msanii Rachel Haule katika enzi za uhai wake
Mchawi kutoka Tanzania ahukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela nchini Kenya baada ya kumdanganya mama mmoja
Unknown 06:59
Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa
kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya
uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta
alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na
hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.
Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela
zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012
baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe
maradufu
Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa
Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa
walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya
kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu
Nairobi.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa
wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa
urahisi na kuwa hawana majuto au toba
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC
Mtoto aliyekuwa amefichwa ndani ya boksi aanza kupumulia Mashine
Unknown 06:55
MTOTO Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka minne mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili .Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipohamishiwa Mei 26 mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika Hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Daktari
bingwa wa Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu alisema
Nasra, aliwekewa mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni
baada ya kuanza kupumua kwa shida.
Alibainisha kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea vizuri lakini
juzi usiku ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.
Dk. Kombo alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu juzi
waliamua kumfanyia vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.
Dk. Kombo, alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa Nemonia,
ataendelea na vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.
Alisema licha ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea kumpatia
chakula na dawa baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.
Ofisa Muuguzi wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya kupumulia
mashine hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia
vipimo kujua maendeleo yake.
Naye mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya mtoto
hajawekewa mashine ya kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na
kiunoni
Mtoto Nasra alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani ambao
walimweleza Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa
alikuwa amefichwa katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la
Mariamu Said mkazi wa Kata hiyo mkoani Morogoro.
Majirani hao walimweleza Zongo kuwa Nasra alifichwa ndani ya boksi
tangu akiwa na umri wa miezi tisa 2009 na kwamba hafanyiwi usafi wala
kumtoa nje.
Jumatatu, 19 Mei 2014
Ajali yaua watano na kujeruhi 16 mlima Senkenke mkoani Singida
Unknown 01:15
WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye Barabara Kuu ya Singida -Mwanza.
Mganga
wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu, alisema
kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati abiria hao wakienda
kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui.
Dk
Mbulu aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva Athuman Adam
(34) na Ally Wambura (36), wakazi wa Igunga na Amin Salim (45) mkazi wa
mjini Singida. Alisema miili ya watu wawili haijatambuliwa.
Kwa
mujibu wa Dk Mbulu, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo
lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo
kasi.
Alisema
kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo,
wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi
huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya.
Baadhi
ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo
ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
Walidai
kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo
akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na
kupinduka mara nne.
Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.
Breaking News:Msanii wa Filamu, Adam Kuambiana afariki dunia
Unknown 01:14
Mwigizaji na Director wa filamu maarufu hapa nchini, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo.
Marehemu alianguka chooni
akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar.
Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na
tumbo.
Marehemu Kuambiana katika muonekano wake wa siku zake za mwisho za uhai wake
Marehemu Kuambiana katika pozi na msanii Irene Uwoya
Marehemu Kuambiana (kushoto) akiwa na wasanii wenzake JB (kutoka kulia), Tino na Mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi
Daktari asahau kitambaa tumboni mwa Mgonjwa mkoani Tabora....Mgonjwa atolewa Kizazi na kukatwa sehemu ya Utumbo ili kukitoa kitambaa hicho
Unknown 01:14
Waziri wa Afya
MKAZI wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mwamini Adamu ametolewa mfuko wa kizazi na kukatwa sehemu ya utumbo baada ya mganga wa idara ya upasuaji katika wilaya hiyo kusahau kitambaa tumboni kwa mwanamama huyo wakati akijifungua.
MKAZI wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mwamini Adamu ametolewa mfuko wa kizazi na kukatwa sehemu ya utumbo baada ya mganga wa idara ya upasuaji katika wilaya hiyo kusahau kitambaa tumboni kwa mwanamama huyo wakati akijifungua.
Kutokana
na kumsababishia ulemavu huo kwa uzembe, Mwamini ameifikisha
Halmashauri ya wilaya ya Urambo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi
akidai fidia ya Sh milioni 500.
Mwamini
ambaye anadai kuwa alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na uzembe wa
uliofanywa na Dk Jacob Kamanda aliyemfanyia upasuaji wakati wa
kujifungua na kumsababishia aondolewe mfuko wa kizazi pamoja na kukatwa
utumbo.
Mwamini
pamoja na mumewe Idrisa Jafari katika madai yao wametaka walipwe fedha
hizo kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wa upasuaji
kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mama huyo.
Akitoa
ushahidi wake mbele ya Jaji Amir Mruma jana, mama huyo alidai kuwa
Januari 6 mwaka 2011 alijifungua kwa upasuaji baada ya hapo hali yake
ilizidi kuwa mbaya huku akitokwa usaha ukeni na sehemu ya tumbo kwenye
mshono.
Huku
akiongozwa na wakili wa kujitegemea Mussa Kwikima, mama huyo aliiambia
mahakama kuwa hali hiyo ilifanya apelekwe hospitali ya mkoa wa Tabora
Kitete bila mafanikio ndipo ikamlazimu kwenda Itigi kwa matibabu zaidi.
Katika
uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na madaktari bingwa, Haile Sales
ambaye ni raia wa Italia pamoja na Anatole Lukonge wa hospitali hiyo ya
Itigi, waligundua kuwa kuna kitu tumboni kama uvimbe hivyo wakalazimika
kumfanyia upasuaji mwingine.
Baada
ya upasuaji huo walikuta kitambaa cha rangi ya kijani ambacho kilikuwa
kimeozesha mfuko wa uzazi pamoja na utumbo kugandana na kitambaa hicho
ikabidi kitambaa hicho kutolewa na kusababisha kupasuka kwa utumbo ili
kumnusuru maisha yake.
Naye
daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama na ambaye ni mganga mkuu wa
hospitali ya Itigi, Anatory Lukonge katika ushahidi wake ameiambia
mahakama hiyo kuwa alimpokea mlalamikaji akiwa anatokwa na usaha ukeni
na sehemu iliyoshonwa.
Dk
Lukonge amebainisha kwamba walipomfanyia upasuaji mama huyo, walikuta
utumbo umeshikana na mfuko wa uzazi huku kukiwa na kitambaa
kimeng’ang’ania juu yake.
Alisema
wakati walipojaribu kukiondoa kitambaa hicho kibofu cha mkojo
kilipasuka wakalazimika kumuwekea mpira ili uweze kumsaidia kutolea
uchafu.
Kesi
hiyo ya madai namba 13/2011 imeahirishwa hadi Agosti tatu mwaka huu
itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake.
Picha za Nusu Uchi za Irene Uwoya akiwa Bafuni zasambaa Kwa Kasi ....
Unknown 01:09
Picha zinazodaiwa kuwa ni mpya za star wa filamu nchini Irene Uwoya akiwa bafuni na taulo na picha nyingine akiwa ameondoa taulo kifuani na kujiziba kwa mikono zimeanza kusambaa mitandaoni kwa kasi.
Uwoya alikuwa kimya kidogo huku habari zake zikiendelea kutawala mitandaoni na magazetini kama kawaida lakini kwa picha hizi inaonekana ametoa ishara kuwa yupo kama kawa...
Kwasasa star huyo yupo nchini Uturuki na wasanii wenzake Vicent Kigosi "Ray", King Majuto na Jacob Stephen "JB" kwa ziara maalum ya kikazi hivyo haijajulikana kama picha hizo zimepigwa akiwa Tanzania au huko Uturuki.
Kupiga picha kwa star akiwa na taulo tu ni jambo la kawaida tu kutegemea picha zimechukuliwaje na kwa lengo gani lakini picha ya Uwoya inayoleta utata hasa ni hiyo aliyoweka mikono kujiziba sehemu ya kifuani na namna alivyojiziba.
Meneja wa Ewura AJINYONGA kwa kutumia Tai hotelini baada ya kuhojiwa na Bunge....Polisi wasema hakupendezwa na maswali ya kamati ya Bunge
Unknown 01:02
Meneja Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) amekutwa amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alihojiwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti.
Meneja huyo, Julius Gashaza, ambaye alikuwa na
jukumu la kupanga bei za mafuta za kila mwezi, alihudhuria kikao hicho
mjini Dodoma kwa siku mbili; Ijumaa na Jumamosi iliyopita kuhusu mambo
mbalimbali, yakiwamo kiwango cha mafuta kinachoingizwa nchini, mgawo wa
fedha unaotolewa na Ewura kwenda kuhudumia umeme vijijini (Rea) na fedha
za mfuko wa barabara.
Jeshi la Polisi, Mkoa wa Temeke limethibitisha
tukio hilo na kueleza kuwa meneja huyo alikutwa amejinyonga kwa kutumia
tai kwenye hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo Vituka wilayani Temeke.
Nyumbani kwa meneja huyo wa Ewura, kulikuwa na
waombolezaji waliokuwa kwenye vikundi na kikao cha maandalizi ya mazishi
kilifanyika ndani ya nyumba ya marehemu iliyopo Yombo Vituka na baadaye
kuhamia nyumba ya jirani.
Kamati ya Bunge ya Bajeti, inayoongozwa na Mbunge
wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ilikutana na maofisa wa Ewura,
akiwamo Gashaza na wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kugundua
kuwapo kwa tofauti katika takwimu za kiwango cha mafuta kilichostahili
kutozwa kodi.
Gashaza alikwenda Dodoma kutoa ripoti ya Ewura
kwenye kamati hiyo ya Bunge akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ewura,
Felix Ngamlagosi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kamati hiyo,
takwimu za Ewura ziliashiria kuwa fedha zilizopatikana ni nyingi zaidi
ya zile zilizoelezwa na TRA, lakini Wizara ya Fedha ilisisitiza zifuatwe
takwimu za mamlaka ya mapato.
Habari hizo, zinasema baada ya kurejea Dar es
Salaam juzi majira ya saa tatu usiku, Gashaza hakwenda nyumbani kwake na
badala yake alikwenda kwenye hoteli iliyo karibu na nyumbani ambako
mkewe na ndugu yake mmoja walimfuata na akawaeleza kuwa anahisi
kutishiwa maisha yake.
Baadaye walifanya maombi maalumu kabla ya kuachana naye.
Inadaiwa kuwa marehemu aliomba akalale hotelini
kwa sababu hakuona kama ana amani kulala nyumbani kwake na ilipofika
asubuhi alikutwa ‘amejinyonga’ ndani ya chumba alicholala hotelini humo.
Nyumbani kwa marehemu waombolezaji walikusanyika
katika makundi, lakini baada ya kukaa katika kikao cha familia walitoka
na kauli moja kuwa hawatasema chochote na kwamba jukumu hilo libaki
mikononi kwa polisi.
Polisi wathibitisha
Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Seleiman Kova
hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo akidai kuwa anayetakiwa
kulizungumzia ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Engbert Kiondo.
Alipotafutwa, Kamanda Kiondo alisema kulingana na
taarifa zilizopo Gashaza aliitwa bungeni Mei 14 na akarejea Dar es
Salaam Mei 17. Alisema aliporejea, Gashaza aliaga nyumbani kwake kuwa
hajisikii vizuri na kuelekea Hoteli ya Mwanga Lodge iliyopo Yombo ambako
alichukua chumba Namba 113.
Kamanda Kiondo alisema akiwa hotelini, Gashaza
alimpigia simu rafiki yake mmoja anayejulikana kwa moja la Silipwango
akimweleza kuwa yupo hotelini hapo kujipumzisha kwa sababu bungeni
aliulizwa mambo ambayo hayakumpendeza na kwamba alihitaji kupumzika.
Rafiki huyo, kwa mujibu wa Kiondo, alimpigia simu
mkewe anayeitwa Judith akamweleza alivyoelezwa na mumewe na baadaye kwa
pamoja wakamfuata hotelini ambako baada ya kuzungumza nao kwa muda
mfupi, aliwaomba wamuache apumzike na ndipo walipoondoka.
Asubuhi, Silipwango alipigiwa simu na mkewe
kumueleza kuwa Gashaza hakurudi nyumbani na akaamua kupitia kwenye
hoteli waliyomuacha na alipofika akakuta watu wamejaa. Alipouliza
akaelezwa kuwa kuna mtu amejinyonga chumbani.
Kamanda Kiondo alisema Gashaza alijinyonga kwa
kutumia tai aliyoifunga kwenye bomba la maji ambalo pia lilikatika na
hivyo kuukuta mwili wake ukiwa sakafuni.
Kilichojiri kamati ya bajeti
“Kisheria kodi ya mafuta ni Sh263 kwa lita
inakwenda mfuko mkuu Hazina na Sh50 inakwenda kwa Wakala wa Umeme
Vijijini (Rea), lakini takwimu za mafuta yaliyouzwa inayostahili kutozwa
kodi kati ya TRA na Ewura zinatofautiana,” alisema mmoja wa wajumbe.
“Kwa hiyo Kamati ya Bajeti iliwaita wote (Ewura na
TRA) na kwa kweli wajumbe wa kamati tulikuwa wakali sana, hatutaki
mchezo tulitaka kujua nani anasema ukweli,” alidokeza mjumbe huyo.
“Uko ugomvi mkubwa tu kati ya TRA na Ewura kuhusu
nani hasa mwenye takwimu halisi,” alisema mjumbe huyo na kudokeza kuwa
meneja huyo alisema kila kitu kwa uwazi.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zimeeleza kuwa
baada ya vuta nikuvute ndani ya kamati hiyo, iliamuliwa watendaji wa
vyombo hivyo viwili wakafanye ulinganisho na kupeleka jibu kwa kamati
hiyo. Ewura waliwasilisha takwimu zao Jumamosi.
“Tension (mvutano) ni kubwa kwa sababu kuna watu
wizarani hawazitaki takwimu za Ewura na wanataka za TRA ambazo sisi kama
wajumbe tunaziona hazina uhalisia kunaweza kukawa na ufisadi,”
alisisitiza mjumbe mwingine.
Chenge azungumza
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew
Chenge alipoulizwa jana, alikiri kufanyika kwa kikao kilichomuhusisha
meneja huyo na kwamba taarifa alizotoa zilionekana tofauti na zile za
TRA.
“TRA ni chombo cha Serikali na Ewura ni chombo cha
Serikali, kwanini wawe na takwimu zinazotofautiana? Hilo tu ndio
tumewaagiza wakae pamoja watuambie zipi ni takwimu halisi,” alisema
Chenge.
Alipoelezwa kuwa mmoja kati ya maofisa wa Ewura
waliofika mbele ya kamati yake amejinyonga, Chenge alionyesha kushtushwa
na kuhoji kama taarifa hizo zina ukweli.
“Una uhakika kwamba amejinyonga? lini? Kama ni
kweli basi ni jambo la kusikitisha sana, lakini hiyo sasa ni kazi ya
polisi. Mimi nisingependa sana kuzungumza, tuwaachie wao wachunguze
sababu za kifo chake,” alisema Chenge.
Serikali inaelezwa kuwa katika hali mbaya kifedha
na kamati hiyo ya Bajeti imekuwa ikifanya kila linalowezekana kuinusuru
kwa kukutana karibu kila siku na Hazina na wadau wengine wanaochangia
fedha katika mfuko wake.
Kwa bajeti ya mwaka 2013/2014 iliyopitishwa na
Bunge, Serikali imejikuta ikiwa na upungufu wa Sh1.8 trilioni hali
ambayo kamati ya bajeti inatafuta kila njia ikiwamo kushauri vyanzo
vipya vya mapato ili kunusuru bajeti ya mwaka huu wa 2014/2015.
Bajeti ambazo zinaelezwa kuiumiza kichwa Serikali
ni ya Maji, Miundombinu na Nishati na Madini ambazo zinaelezwa kupata
mgawo kidogo mwaka jana na kuzifanya zishindwe kutekeleza miradi
mbalimbali.
Mkurugenzi wa Petroli wa Ewura, Godwin Samwel alisema alipata taarifa jana saa 3:00 asubuhi.
Alithibitisha kuwa marehemu alikuwa Dodoma kikazi kwenye vikao na kamati ya Bunge tangu Alhamisi iliyopita.
Baada ya kumaliza kazi ndiyo ndiyo jana (juzi)
alichelewa sana kurudi ndipo alipoamua kujipumzisha kwenye nyumba ya
wageni (iliyopo karibu na nyumbani kwake) ambako alikutwa amefariki,”
alisema Samwel.
Alisema marehemu alikuwa mwadilifu, mchapa kazi na asiye na tatizo lolote kazini na kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa.
Credit: Mwana
Credit: Mwana