Jumatatu, 19 Mei 2014

Breaking News:Msanii wa Filamu, Adam Kuambiana afariki dunia



Mwigizaji  na Director  wa  filamu maarufu   hapa  nchini, Adam Kuambiana amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa matibabu alfajiri ya kuamkia leo. 

Marehemu alianguka chooni akiwa location katika hoteli ya Silver Rado iliyopo Sinza kwa Remy, Dar. Kabla ya mauti kumfika, Adam alikuwa akilalamika kuwa anasumbuliwa na tumbo.
Marehemu Kuambiana katika muonekano wake wa siku zake za mwisho za uhai wake
Marehemu Kuambiana  katika pozi na msanii Irene Uwoya
Marehemu Kuambiana (kushoto) akiwa na wasanii wenzake JB (kutoka kulia), Tino na Mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi

0 maoni:

Chapisha Maoni