Mchawi kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana Amos Chipeta pia ataongezwa
kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa vinavyoumiwa kufanya
uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.
Kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta
alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana Peter Christopher aliyepatikana na
hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.
Bwana Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela
zake tarehe tofauti tofauti kati ya mwezi wa Agosti na Decemba 2012
baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba wazifanye pesa hizo ziwe
maradufu
Walijitetea kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa
Maafisa wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa
walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari 1, 2014 katika nyumba ya
kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa mji mkuu
Nairobi.
Hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa
wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa mjinga na basi kumnafiki kwa
urahisi na kuwa hawana majuto au toba
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC
0 maoni:
Chapisha Maoni