Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahamani Kinana akiongozwa na Mkuu wa Moa wa
Singida Dk, Parseko Kone, Katibu Tawala Lianna Hassan na viongozi
wengine wa Mkoa wa Singida kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa
hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, wakati Kinana alipokuwa Mkoani
Singida kwa ziara ya kikazi ya siku saba.
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone amesema serikali imetoa zaidi
ya shilingi 6.7 bilioni kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa hospitali ya
rufaa ya mkoani hapa iliyoko kijiji cha Madewa nje kidogo ya Singida
mjini.
Dk.Kone amesema hospitali hiyo itakapokamilika,itahudumia wagonjwa kutoka mikoa yote ya kanda ya kati.
Mkuu
huyo alitoa rai hiyo wakati akitoa akitoa taarifa yake kwa katibu mkuu
CCM taifa,Abrahamani Kinana aliyetembelea hospitali hiyo hivi karibuni.
Amesema
mkoa umetegewa eneo la ekari 283 kwa ajili ya uendelezaji wa mradi wa
hospitali hiyo, ambayo itakuwa ya mfano hapa nchini.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Dorothy Gwajima amesema
lengo la mradi huo ni kuimarisha huduma za afya mkoani pamoja na mikoa
jirani.
Katibu Mkuu wa CCM akiweka saini kwenye kitabu cha hospitali ya Rufaa
huku Naibu Katibu Mkuu wake Mwigulu Nchemba na mkuu wa Mkoa wa Singida
Kone wakishuhudia.
Dk.Gwajima amesema mradi huo utakapomalizika,utakuwa na majengo 29 yatakayotumika kutoa huduma mbali mbali.
Mganga
huyo mkuu,amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na uhaba wa
watumishi,nyumba za kuishi watumishi na ufinyu mdogo wa bajeti ya dawa
kutoka bohari kuu ya madawa (MSD).
Kwa
upande wake Kinana,alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk.Kone kwa utendaji
kazi wake ambao umesaidia kujengwa kwa hospitali hiyo.
Mganga mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Singida (RMO) Bi. Doroth Bwajima akisoma taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo.
Amesema baada ya mradi huo kukamilika mkoa wa Singida utaondokana na matatizo ya huduma za afya.
"Ili
kumuunga mkono Dk.Kone kwa hili jambo nzuri la ujenzi wa hospitali ya
rufaa ambayo itasaidia Watanzania wengi kupata huduma ya afya kwa
kiwango kizuri,nitahakikisha nina muunganisha na baadhi ya marafiki
zangu wa ndani na nje ya nchi ili waweze kusaidia kumalizika kwa ujenzi
wa hospaitali hii inayovutia",amesema Kinana.
Mganga mfwawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Dkt Joseph
Malunda, akiwaonesha michoro ya hospitali hiyo viongozi walioambatana na
Kinana.
Viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakimsikiliza Dkt Malunda.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai akisisitiza jambo kwa Kinana.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida Pendael Maasai
akimwonyesha Katibu Mkuu kinana vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye
hospitali hiyo ya rufaa.
Mbunge MO akiangalia mojawapo ya vifaa vya hospitali ya rufaa ya singida.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji akisalimiana na Daktari bingwa
wa magonjwa ya kina mama wa mkoa wa Singida Dkt, Seleman Mutani wakati
wa ukaguzi wa hospitali hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa akiongozana na mkuu wa Mkoa Kone, Mbunge wa jimbo la
Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji, wasaidizi wa Mbunge Duda Mugheny na
David Mkufya wakimwongoza Kinana kutoka nje mara baada ya kukagua
hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo.(Picha zote na Zainul Mzige wa
modewjiblog).
DKT. BILAL AZINDUA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI NA MFUKO WA ELIMU WA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohameed Gharib Bilal,
akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani,
wakati alipofika kwenye Kambi ya JKT Ruvu kwa ajili ya kupanda miti
ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo, ambapo jumla ya miti 8,000, imeandaliwa
kupandwa katika eneo hilo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipanda mti katika eneo la Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu,
ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya mazingira Duniani. jumla ya miti
8,000 inatarajia kupandwa katika eneo hilo.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza, akipanda mti katika eneo la Kambi ya
Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya
mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo
hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiweka Jiwe la msingi baada ya kupanda mti katika eneo la Kambi ya
Jeshi la Kujenga Taifa, JKT Ruvu, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa Wiki ya
mazingira Duniani. jumla ya miti 8,000 inatarajia kupandwa katika eneo
hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi wa kambi ya JKT Ruvu
baada ya kupanda miti.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walio katika mpango
maalum wa kampeni ya upandaji miti hiyo, baada ya kupanda miti.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walio katika mpango
maalum wa kampeni ya upandaji miti hiyo, baada ya kupanda miti.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodi ya Wadhamini
ya Mfuko wa Hifadhi ya Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF)baada ya
kupanda miti.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya maafisa wa Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT
Ruvu, wakati akiondoka eneo hilo baada ya kupanda miti kama ishara ya
uzinduzi wa Wiki ya Mazingira Duniani, leo
Vijana wa JKT wakitoa burudani ya ngoma ya "Msewe" toka Zanzibar
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri
ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kibaha
Mailimoja le
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akivishwa Skafu na vijana wa Scout wa mji wa Kibaha, wakati alipowasili
kwenye uwanja wa Mailimoja Kobaha, kwa ajili kuzindua Mfuko wa Elimu wa
Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani, leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisimama na viongozi waliokuwa meza kuu kwa ajili ya kupokea
maandamano ya wanafunzi wakati wakiingia kwenye uwanja huo leo wakati wa
uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoa wa
Pwani, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mailimoja Kibaha.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na Sekondari za mkoa wa
Pwani, wakipita mbele ya jukwaa kuu na Mabango yenye ujumbe mbalimbali
kuhusu suala zima la elimu, wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa
Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoa wa Pwani, iliyofanyika kwenye Uwanja
wa Kibaha Mailimoja leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi cheti cha shukrani, Mbunge wa Jimbo la Kibaha, Silvester
Koka, kwa kutambua mchango wake katika kuchangia Mfuko wa Elimu, wakati
wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha
mkoa wa Pwani, iliyofanyika leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi cheti cha shukrani, mwakilishi wa Kampuni ya Lemita Ltd,
Mgeta Mganga, kwa kutambua mchango wake katika kuchangia Mfuko wa Elim,
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa
Kibaha mkoa wa Pwani, iliyofanyika leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi cheti cha shukrani, mwakilishi wa NSSF, Ummy Lweno, kwa
kutambua mchango wake katika kuchangia Mfuko wa Elimu, wakati wa hafla
ya uzinduzi wa Mfuko wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoa wa
Pwani, iliyofanyika leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati akiwasili uwanjani hapo.
Baadhi
ya wananchi na wanafunzi wa mji wa Kibaha wakichangia kwa hiyari mfuko
wa Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa
Elimu wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoa wa Pwani, uliofanyika kwenye
Uwanja wa Mailimoja Kibaha. Picha na OMR
0 maoni:
Chapisha Maoni