Wapiganaji wanaoshukiwa kuwa wanachama wa Boko Haram wamewateka nyara wanawake 20 kutoka jamii inayohamahama Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wanawake hao walichukuliwa katika Makazi ya
Gakini Fulani karibu na mji wa Chibok ambako zaidi ya wasichana
wanafunzi 200 walitekwa nyara Aprili, mwaka huu.
Walioshuhudia tukio hilo walisema
kuwa wapiganaji hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki waliwalazimisha
wanawake hao kuingia katika magari yao kabla ya kutoroka nao katika
Jimbo la Borno.
Mlinzi mmoja wa kijiji alisema kuwa washambulizi
hao pia waliwateka nyara wanaume watatu waliojaribu kuwazuia wasiondoke
na wanawake hao. Hadi sasa jeshi halijasema lo lote kuhusiana na tukio hilo.
Katika hatua nyingine, jeshi la Nigeria limesema kuwa
limewaua wapiganaji 50 katika kampeni yake dhidi ya magaidi mwishoni mwa
wiki katika majimbo ya Borno na Aladawa.
Mfululizo wa mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo umeimarisha ukosoaji wa vyombo vya usalama vya Serikali.
Licha
ya kuwepo kwa hali ya hatari katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria wanajeshi hawajachukua hatua thabiti kukabiliana na hali
hiyo.
Chanzo: BBC
Chanzo: BBC
0 maoni:
Chapisha Maoni