Jumapili, 1 Juni 2014

Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kosa la kuolewa na mkristo kuachiwa huru hivi karibuni


Mwanamke wa Sudan anayesubiri hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuolewa na Mkristo huenda akaachiwa huru hivi karibuni.
 
Afisa mmoja wa serikali amesema nchi hiyo inaendelea na mipango ya kumwachia Meriam Ibrahim katika siku chache zijazo.
 
Meriam Ibrahim aliyebadili dini na kuwa Mkristo anakabiliwa na hukumu ya kifo kwa kukataa kurudi tena katika dini ya Kiislamu.

Meriam alijifungua mtoto wake wa pili akiwa gerezani Jumatano iliyopita katika ndoa ambayo imedumu tangu mwaka 2011 na mumewe Daniel Wani raia wa Marekani.
 
Kwa mujibu wa afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Sudan amesema mwanamke huyo ana haki ya kufuata kile anachotaka kwa sababu sheria ya Sudan inawakubalia watu kuamini kile wanachokitaka.
 
Wakili wa Meriam, pamoja na mumewe wamesema hawajafahamishwa chochote kuhusiana na mipango ya kuwachiliwa huru kwake.
 
Mahakama ilisema Meriam angeweza kumuhudumia mtoto wake kwa miaka miwili kabla ya hukumu yake.
 
Sudan ina idadi kubwa ya Waislam na sheria za kiislamu zimekuwa zikipewa uzito tangu mwaka 1980.

0 maoni:

Chapisha Maoni