Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya Tamko kwa Vyombo vya Habari juu ya Chaguzi za
Afrika Kusini na Malawi uliofanyika mapema huu. Mkutano huo wa waandishi
wa habari ulifanyika mwishoni mwa wiki katika ofisi za Jukwaa La Katiba
zilizopo Sinza Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba akitia msisitizo juu ya Tamko kwa
Vyombo vya Habari juu ya Chaguzi za Afrika Kusini na Malawi uliofanyika
hivi karibuni.
Hali ya uchaguzi ilivyokuwa nchini Africa Kusini na Malawi ni kama ifuatavyo;
Picha
inaonyesha mwanachama aliyevaa flana yenye nembo ya chama cha ANC cha
Afrika Kusini siku ya uchaguzi. Hii ni sawa na kupiga kampeini siku ya
uchaguzi kitendo ambacho ni kinyume na sheria za
uchaguzi.
Picha
inaonyesha wapiga kura nchini Malawi wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura
eneo la wazi ikimanisha jua na mvua vinaweza vikaathiri mchakato pia
sehemu ya kupigia kura ipo kwenye ngazi kwahiyo siyo
mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu na wazee.
0 maoni:
Chapisha Maoni