Alhamisi, 12 Juni 2014

Vurugu kubwa zaibuka jijini Mwanza, Mabomu ya machozi yarindima kila kona...Barabara, maduka yafungwa



JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo  maarufu  kama  machinga waliokuwa wakipinga kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini Mwanza. ...
 
Hatua hiyo imesababisha vurugu kubwa na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara zinazokatiza katikati ya jiji  kuanzia saa nne asubuhi ....
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Valentino Mlowola, amedai  kuwa Jeshi hilo limelazimika kutumia mabomu hayo ili kuwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wakihatarisha amani na kwamba  hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo. 
 

0 maoni:

Chapisha Maoni