Wanawake wanne raia wa Rwanda wametiwa mbaroni mjini Dodoma kutokana na kuingia nchini kinyemela na kujihusisha na biashara ya ukahaba.
Watuhumiwa
watatu kati ya hao, Saidat Umotoni (28), Asha Abimana (25) na Asia
Umotoni Wase (30), hii ni mara yao ya pili kukamatwa mjini hapa
wakidaiwa kujihusisha na biashara hiyo.
Mara
ya kwanza ilikuwa Novemba mwaka jana ambapo wote ( Asia, Asha na
Saidat) baada ya kukamatwa, walirudishwa kwao baada ya kulipa faini.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Kaimu Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dodoma,
Proches Kuoko, alimtaja mwingine aliyekamatwa ni Chalote Uwase (28)
ambaye ameshahukumiwa kifungo cha miaka miwili anachotumikia katika
Gereza la Isanga, mjini hapa.
Alisema
wahamiaji hao wote kwa pamoja walikamatwa na maofisa wa kikosi cha
Uhamiaji, baada ya kupata taarifa kwa kuwepo raia hao katika eneo la
barabara ya Bahi ndani ya Manispaa ya Dodoma.
Alisema
wanawake hao walikamatwa usiku kwenye mitaa hiyo huku wakiwa kwenye
harakati za kutafuta wateja na walipohojiwa wote kwa pamoja hawakuwa na
hati ya kusafiria na kuishi hapa nchini na walizokuwanazo zilikuwa
zimeisha muda wake wa matumizi.
“Hata
walipopekuliwa, walikutwa wakiwa na hati ya kusafiria iliyokuwa
imeisha muda wake wa kuwawezesha kuishi hapa nchini na walipohojiwa
zaidi walisema wao kazi yao ni uchangudoa,”alisema Kuoko.
0 maoni:
Chapisha Maoni