Jumapili, 1 Juni 2014

Breaking News: Mama mzazi wa Zitto Kabwe afariki dunia


Rais Jakaya Kikwete alipomjulia hali Mama Mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA Zitto Zuberi Kabwe aliyekuwa amelazwa katika wodi ya wagonjwa wenye kuhitaji uangilizi maalumu (ICU) katika hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam hivi majuzi. (picha: Freddy Maro/IKULU)
**********

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (CHAWATA), Shida Salum, ambaue alikuwa mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, aliyekuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani, amefariki  dunia. 

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari  mbalimbali, bi. Shida alianza kusumbuliwa na maradhi ya saratani mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu akiwa mjini Dodoma akisubiri kuapishwa pamoja na wajumbe wengine wa Bunge Maalumu la Katiba.


Zitto alinukuliwa akisema kuwa, baada ya hali ya mama yake kuwa mbaya alishindwa kuendelea kukaa Dodoma kusubiri kuapishwa na alipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambako aligundulika kuwa na saratani ya shingo ya kizazi na kupatiwa tiba kwa mwezi mmoja kabla ya kupelekwa India kwa matibabu zaidi.

Alisema kabla ya kupelekwa hospitalini hapo, alikuwa akiendelea kupata matibabu akiwa nyumbani, lakini hali yake ilibadilika juzi.

Zitto, ingawaje alisema hali ya mama yake haikutengemaa tangu aanze kusumbuliwa na maradhi hayo, alikuwa na matumaini: “Hali ya mama kwa kweli siyo nzuri, lakini nina imani itakuwa nzuri na kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa kama zamani,” alisema Kabwe ambaye alidai kuwa kutokana na maradhi hayo ya mama yake, alishindwa kuhudhuria Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma.


Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). 


Viongozi na wasanii mbalimbali wametuma salamu za pole kwa Zitto Kabwe.

Bernard Membe
Zitto kabwe pole sana kwako na ndugu kwa Msiba huu mzito. Tunawaombea subira na Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi..Amina

 
William Ngeleja
Nimepokea Taarifa za msiba wa Bibi Shida Salum(mama mzazi wa Mhe. Zitto Kabwe) kwa masikitiko makubwa. Nawapa pole familia nzima ya ndugu yetu Zitto katika kipindi hiki cha Majonzi. Mwenyezi Mungu awape Wepesi , na Pia natoa pole kwa wote walioguswa na Msiba wa George Otieno aliyefariki Jana. Tuendelee kuziombea familia hizi na zingine zenye misiba ili wapate faraja kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni mfariji Mkuu!

 
Jokate Mwegelo
Zittokabwe I’m so so sorry Zitto. May her soul rest in peace. Amen!!

 
Linex Sunday
Nachukua nafasi hii kuipa pole familia ya Zitto Ruyagwa Kabwe Ndugu jamaa Marafiki kwa kumpoteza Bi Shida Mungu awape nguvu katika kipindi hichi kigumu R.I.P Bi shida tulikupenda lakini Yeye aliyekuleta amekupenda zaidi Jina LA Bwana libalikiwe na mapenzi yake yatimie.

 
Kupitia  Ukurasa wake  wa  Twitter,Zitto  Kabwe  ameandika:

0 maoni:

Chapisha Maoni