Mrembo aliyeonekana kwenye picha inayodaiwa kutengenezwa kitaalam akiwa na mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapten John Komba, anasakwa kwa udi na uvumba....
Kusakwa
kwa mwadada huyo anayedaiwa kuishi maeneo ya Kinondoni jijini
Dar es salaam, kumekuja siku chache tangu mbunge huyo atoe
taarifa kwamba hauhusiki na picha hizo na ana imani kwamba
zimetengenezwa na wabaya wake....
Inaaminika kwamba kupatikana kwa mwanamke huyo kutategua kitendawili kuhusiana na tukio hilo.
Taarifa
iliyotolewa na mbunge huyo ilisema kwamba picha hizo
zimetengenezwa na maadui wake wa kisiasa na kwamba yeye siyo
kiongozi wa hovyo hovyo namna hiyo....
Komba
alisema kwamba anawakaribisha wataalamu wa picha na mitandao
kuthibitisha ukweli wa picha hizo kama zinamhusu.
Mbunge
huyo alihoji, iweje awe kwenye mapenzi kama picha hizo
zinavyoonesha halafu awe na nguo zake zote huku msichana akiwa
na kanga tu?
Kapteni
Komba alisema kama taifa limefikia hatua ya kuchafuana sababu
ya mitizamo tofauti ya kisiasa juu ya namna ya kuongoza taifa
letu basi tumefika pabaya sana....
Alisema
wale wote wanaomuamini kama kiongozi shupavu wasikatishwe tamaa
na wachache wenye mawazo ya kitumwa ambao wanadhani wanaweza
kummaliza kisiasa kwa kumtengenezea picha chafu kama hizo...
Katika
hatua nyingine, wadau mbalimbali wameomba kusakwa kwa mtu
aliyezitengeneza na kuzitoa picha hizo kwenye mitandao ya
kijamii ili ahojiwe...
Wadau
hao walisema, mtu huyo akipatikana na kuhojiwa ndipo
itajulikana nini kilikuwa chanzo cha kufanya jambo hilo .
0 maoni:
Chapisha Maoni