Ili
kuwa ni hafla ya aina yake iliyojaa tabasamu, kukumbatiana na maneno
ya " welcome back, good to see you again, we have missed you"
yakitawala wakati Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Dkt.
Asha- Rose Migiro alipofika Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon na kisha kukutana na kubadilishana mawazo na
Katibu Mkuu mwenyewe wakianza na mazungumzo ya faragha kati yao wawili
na kisha kujumuika na wafanyakazi wa Ofisi Binfasi ya Katibu Mkuu na
Ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu. baada ya Mazungumzo yake na Katibu
Mkuu, Dkt. Migiro pia alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu
Mkuu aliyemwachia kijiti Bw. Jan Eliasson.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na Dkt. Asha-Rose Migiro (
Mb) Naibu Katibu Mkuu Mstaafu na ambaye sasa ni Waziri wa Sheria na
Masuala ya Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati
alipotembeleza Katibu Mkuu jana Jumatatu. Hii ni mara ya kwanza kwa
Dkt. Migiro kufika Umoja wa Mataifa tangu alipostaafu Unaibu Katibu
Mkuu miaka miwili iliyopita. Kabla ya Viongozi hao wawili kupiga
picha hii rasmi, walikuwa na mazungumzo ya faragha ( Tete a tete).
Waziri Migiro yupo hapa Umoja wa Mataifa kuhudhuria Mkutano ulioitishwa
na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za
Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya
2015.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na timu yake akiwa katika
mazungumzo na Dkt. Asha- Rose Migiro ambaye alifuatana na Muwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi
na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi. Katika mazungumzo hayo, Katibu
Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua
Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri
anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na
mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa. Ban Ki Moon
alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake
kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba
amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa.
Ban Ki Moon akiagana na Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya mazungumzo yao.
Baada
ya kuagana na Katibu Mkuu , Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dkt. Asha-Rose
Migiro alielekea ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu Bw. Jan Eliasson ambako
nako kulikuwa na kukaribisha na tabasamu za akina yake. na kisha wakawa
na mazungumzo ya faragha.Pichani ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson
akimkaribisha kwa furaha Dkt. Asha- Rose Migiro ofisi kwake kwa
mazungumzo.
Wakipata picha ya pamoja.
Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson akiwa na Dkt. Asha-
Rose Migiro. Bw. Eliasson alimueleza Naibu Katibu Mkuu Mstaafu kwamba
anajitahidi kufuata nyayo zake na kwamba anapenzi makubwa sana na
Tanzania na Afrika kwa Ujumla, Bw. Eliasson aliwahi kufanya kazi
Tanzania kama mwanadiplomasi chini ya Uongozi wa Rais wa wakati huo
wa Sweden Marehemu Olof Palme.
Dkt.
Asha- Rose Migiro akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
Bw. Jan Eliasson ( Leo jumanne ) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba
Dkt. Asha- Rose Migiro ( Mb) atakuwa miongoni wa wanajopo ( Panellist)
watakaoendesha majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na
utawala wa sheria katika uungaji mkono juhudi za kitaifa na kimataifa
katika kuutokomeza umaskini na maendeleo endelevu. Majadiliano hayo ni
sehemu ya mkutano wa siku mbili ambao umeitishwa na Rais wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. John Ashe na kufunguliwa na Katibu Mkuu
Ban Ki Moon.Kushoto ni Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Balozi
Tuvako Manongi
Naibu
Katibu Mkuu Mstaafu akipokea shada la Maua kutoka kwa mmoja wa
wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Katibu Mkuu. Ujio wa Dkt Migiro,
uliamsha shamra shamra zaina yake kutoka kwa Katibu Mkuu mwenyewe ambaye
kila wakati alikuwa akiachia tabasamu pana, Baraza lake la Mawaziri
pamoja na wafanyakazi wa ofisi yake Binafsi pamoja na ofisi Binafsi ya
Naibu Katibu Mkuu.
" Hili UA zito ngoja tukupokee" ndivyo wanayoelekea kusema Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Mkuu wake wa Itifaki.
"welcome
back" ndivyo anayosema afisa huyu wakati wakisalimia kwa furana ha
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dkt- Asha-Rose Migiro huku Katibu Mkuu
akiangalia kwa furaha.
Ilikuwa ni furaha tupu kwa kweli salamu zikiendelea
0 maoni:
Chapisha Maoni