Jumanne, 10 Juni 2014

Nick Minaj ayaanika Maziwa yake Jukwaani


Mwanamziki  Nick  Minaj  mwishoni  mwa  wiki  jana  alifanya  tukio  la  kushangaza  baada  ya  kuamua  kuonesha  matiti  yake  wakati  akitumbuiza  jukwaani  katika  tamasha  la  muziki  la  Summer  Jam  Hip-Hop  lililofanyika  New  Jersey  nchini  Marekani  ambako  wasanii  kadhaa  wa  Hip Hop  walitumbuiza.....

Minaj  alipanda  jukwaani  hapo  huku  akiwa  amevalia  suruali  ya  kubana, kwa  juu  alivalia  kiblauzi  cha  kupwaya  kilichoacha  wazi  sehemu  kubwa  ya  tumbo  lake  kutokana  na  kushonwa  kwa  kuishia  kwa  chini  ya  matiti  yake  na  zaidi  kilishonwa  kwa  kutumia  kitambaa  cha  kuonesha.....

Wakati  mwanamziki  huyo  akianza  kuimba  aliwashangaza  wengi  waliokuwa  katika  onesho  hilo  kutokana  na  kuanza  kukifunua  kiblauzi  chake  hicho  mara  kadhaa  na  kuwaonesha  mashabiki  wake  matiti  yake  ambayo  kwa  ndani  hayakivishwa  sidiria.

0 maoni:

Chapisha Maoni