Jumanne, 10 Juni 2014

Fahamu Gari la Kifahari la Nay wa Mitego alilojinunulia kama zawadi ya Birthday pamoja na Umri wake kwa sasa


Jana June 9 Nay wa Mitego alisharehekea siku yake ya kuzaliwa ikiwa ni mwaka wake wa mafanikio zaidi katika muziki.
 
Nay ameweka wazi kuwa amefikisha umri wa miaka 29 na kwamba ameamua kufanya birthday party kwa mara ya kwanza tangu azaliwe, na pia amejinunulia zawadi ya gari la kifahari lenye thamani ya shilingi milioni 36. Kibongobongo ni pesa ndefu.
 
“Nimejinunulia gari aina ya Murano nafikiri ndio gari yangu ambayo leo ntakuwa nayo na ndio birthday yangu. Inagharimu milioni 36, hii ni ya mwaka 2007…bado mpya bado inadai. one love kwa mashabiki wangu.”
 
Kwa maelezo ya Nay wa Mitego, hii ndio aina ya gari alilonuanua, Murano ya mwaka 2007.

0 maoni:

Chapisha Maoni