Alhamisi, 12 Juni 2014

US drones 'hit militants in Pakistan's North Waziristan'


Pakistani tribesmen clear rubble and belongings from their destroyed houses following Pakistan military airstrikes against suspected Taliban hideouts in Miranshah in North Waziristan on 24 May 2014. Pakistan has carried out intensive airstrikes in the North Waziristan region in recent weeks
The US has resumed its drones programme in Pakistan, with two strikes on militant strongholds in the North Waziristan tribal region overnight.
Reports say at least 16 suspected militants were killed in the strikes.
It come days after militants attacked Karachi international airport, killing 39 people, including 10 attackers.
Washington agreed to suspend its drones programme in December to allow Islamabad to pursue peace talks with the Pakistani Taliban (TTP).
But pressure has been mounting on the Pakistani authorities to launch a ground offensive on the region amid a breakdown in peace talks.
Double hit The two drone strikes took place within hours of each other, striking a compound in a village near Miranshah, the main town in North Waziristan.
The first attack, carried out late on Wednesday night, is said to have killed four ethnic Uzbek militants and two Punjabi Taliban.
The second attack on Thursday morning targeted another 10 suspected militants.
Internally displaced Pakistanis arrive in Bannu, a town on the edge of Pakistan's lawless tribal belt of Waziristan, on 11 June 2014. Thousands of people have fled the region amid fears of a widescale military offensive against the militants
On Wednesday, Uzbek militants of the Islamic Movement of Uzbekistan (IMU) claimed to have carried out the attack on the airport, saying it was in retaliation for military air strikes.
The group, which is highly-trained and has bases in North Waziristan, has previously carried out large-scale co-ordinated attacks with al-Qaeda and Taliban militants in Pakistan.
Washington uses unmanned drones to carry out strikes on Taliban and al-Qaeda targets in Pakistan's border region with Afghanistan.
However, US strikes have not taken place since 25 December 2013 in response to calls by Pakistan to halt strikes and enable peace negotiations.
Pakistan launched air strikes against Pakistan's north-west Khyber region, killing at least 15 militants on Tuesday.
line
Who are the Pakistani Taliban?
• With its roots in the Afghan Taliban, the Pakistani Tehreek-e-Taliban movement came to the fore in 2007 by unleashing a wave of violence
Getty Images  
Former TTP leader Hakimullah Mehsud died in a drone strike
• Its leaders have traditionally been based in Pakistan's tribal areas but it is really a loose affiliation of militant groups, some based in areas like Punjab and even Karachi
• The various Taliban groups have different attitudes to talks with the government - some analysts say this has led to divisions in the movement
• Collectively they are responsible for the deaths of thousands of Pakistanis and have also co-ordinated assaults on numerous security targets
• Two former TTP leaders, Baitullah Mehsud and Hakimullah Mehsud, as well as many senior commanders have been killed in US drone strikes
• It is unclear if current leader Maulana Fazlullah, who comes from outside the tribal belt, is even in Pakistan, but he has a reputation for ruthlessness

Vurugu kubwa zaibuka jijini Mwanza, Mabomu ya machozi yarindima kila kona...Barabara, maduka yafungwa



JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo  maarufu  kama  machinga waliokuwa wakipinga kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini Mwanza. ...
 
Hatua hiyo imesababisha vurugu kubwa na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara zinazokatiza katikati ya jiji  kuanzia saa nne asubuhi ....
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Valentino Mlowola, amedai  kuwa Jeshi hilo limelazimika kutumia mabomu hayo ili kuwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wakihatarisha amani na kwamba  hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo. 
 

Soko la Karume lilivyoteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo



Hali ilikuwa tete usiku wa kuamkia leo katika mabanda ya Wamachinga eneo la Soko Karume , Ilala jijini Dar  baada ya kutokea moto mkuwa na kuteketeza mabanda yote ya wafanyabiashara eneo hilo. 
Fire walifika katika eneo la tukio na kuondoka baada ya kukubali kushindwa kuzima moto huo. Nguzo za umeme zimeungua pia.
 
Chanzo  cha  moto  huo kinadaiwa kuwa ni sehemu ya Mama ntilie ambao inasemekana huchemsha maharage na kuyaacha usiku ili yaive vizuri.

Jumatano, 11 Juni 2014

Bajeti kuu ya Serikali itasomwa leo Bungeni Dodoma....Watanzania wasubiria bidhaa zitakazopanda na kushuka, Wafanyakazi nao wasubiria mishahara mipya


Watanzania leo wanaelekeza macho na masikio yao mjini Dodoma, kusikiliza Hotuba ya Bajeti ya Serikali, inayotarajiwa kusomwa saa 10 kamili bungeni na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum.
 
Tayari Waziri Saada alishaeleza kuwa makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2014/15, unaoanza Julai mwaka huu, yatakuwa Sh trilioni 19.6 kutoka makadirio ya Sh trilioni 18.2 ya Bajeti inayoisha muda wake.
 
Vipaumbele vya Bajeti hiyo, kwa maana ya miradi itakayozingatiwa zaidi, ni iliyo katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) unaohusisha sekta sita za Kilimo, Elimu, Maji, Utafutaji rasilimali fedha, Nishati, Uchukuzi na Uboreshaji wa Mazingira ya kufanyia biashara na Mpango wa Maendeleo ya Miaka Mitano.
 
Akisoma mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2014/2015, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wassira, alisema mapendekezo ya mpango huo, yana vipaumbele vitano.
 
Cha kwanza ni miundombinu, kikifuatiwa na kilimo, viwanda vinavyotumia malighafi za ndani na kuongeza thamani, maendeleo ya rasilimali watu na ujuzi na uendelezaji wa shughuli za utalii, biashara na fedha.
 
Katika hotuba hiyo, Watanzania wengi watakuwa makini kusikiliza bidhaa na huduma zitakazoongezwa kodi, jambo linalotarajiwa kuongeza bei ya bidhaa za huduma husika katika soko.
 
Katika bajeti inayoishia,  Serikali iliongeza kodi kwenye magari makuukuu, bia, vinywaji vikali na baridi ambavyo kodi imekuwa ikiongezwa kila mwaka na kuwaathiri watumiaji.
 
Kutokana na hali hiyo wanywaji pombe na sigara baada ya bajeti ya mwaka juzi ya 2012/2013, walilazimika kutumia fedha nyingi ili kupata huduma hizo kwa kiwango kile kile katika mwaka huu wa bajeti unaoisha.
 
Bidhaa zisizokuwa za mafuta ambazo zilifanyiwa marekebisho na kuongezwa kodi ni mvinyo, pombe, vinywaji vikali, na sigara.
 
Ushuru pia uliongezwa kwenye magari yasiyokuwa ya uzalishaji na yenye umri wa miaka 10 kutoka asilimia 20 mpaka asilimia 25.
 
Lengo la Serikali katika hilo, lilikuwa kupunguza uagizaji wa magari chakavu ili kulinda mazingira na kupunguza ajali za mara kwa mara.
 
Katika bajeti hiyo, vijana wa bodaboda walicheka baada ya Serikali kusamehe ushuru wa barabara kwa pikipiki hizo za biashara.
 
Moja ya kivutio kikubwa cha Bajeti inayowasilishwa leo, ni matarajio ya wafanyakazi kuhusu utekelezaji wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa katika sherehe za Mei Mosi mwaka huu, ya kuongeza mshahara wa kima cha chini na kupunguza kodi ya mshahara (PAYE).
 
Rais Kikwete alisema Serikali itaendelea kuongeza mshahara wa kima cha chini na kubainisha kuwa mwaka 2005 alipoingia madarakani, alikuta mshahara wa kima cha chini ni Sh 65,000 na kukipandisha taratibu hadi kufikia Sh 240,000 cha sasa.
 
Kuhusu kupunguza PAYE, Rais Kikwete alisema kusudi la Serikali ni kupunguza kodi hiyo ya mshahara kutoka asilimia 13 inayotozwa sasa, ifikie katika kiwango cha tarakimu moja.
 
Kuhusu misamaha ya kodi ambayo mwaka huu imekuwa gumzo bungeni, huku wabunge wengi wakitaka ipunguzwe, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alinukuliwa akisema wafanyabiashara na vigogo wanaokwepa kodi kwa kujificha kwenye mwavuli wa misahama, hawako salama.
 
“Tutafuatilia kikamilifu kwa kuwa wapo watu wanaingiza bidhaa wanapewa msamaha, lakini ukija kwenye huduma za jamii unakuta bidhaa hizo zinauzwa kibiashara,” alisema.

Mwigulu pia alizungumzia ukwepaji kodi na matumizi mabaya ya fedha za Serikali na kufafanua kuwa, yatadhibitiwa.

“Bahati nzuri niliyonayo, sikuzaliwa na chembe ya woga, kwa hiyo kwenye hili hakuna mkubwa wala mdogo, hakuna mtu atagusa fedha ya umma kwa kukwepa au kwa kutumia vibaya kodi ambayo ilishakusanywa halafu akapona asiguswe,” alisema.

Mwigulu alisema katika Bajeti ya Serikali ya 2014/2015, yapo mambo ya msingi matano, ambayo yatasimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha utekelezaji wake unakuwa tofauti na zilizopita.
 
Mbali na kuondoa misamaha ya kodi, pia makusanyo ya ndani yatatiliwa mkazo zaidi ili kujenga uwezo wa kujitegemea wenyewe badala ya kutegemea wahisani.

Jambo la tatu alisema ni kuhakikisha Serikali inapeleka fedha kwenye mahitaji muhimu na kwa wakati, ili fedha za maendeleo zitumike kama ilivyokusudiwa.

Jambo la nne litakalozingatiwa kwa mujibu wa Mwigulu, ni usimamizi wa fedha zinazopatikana kwani pamoja na makusanyo kidogo, lakini pia kuna uvujaji.

“Tunataka fedha inayopatikana na kupangiwa kazi fulani itumike kwa shughuli iliyokusudiwa. Tutahakikisha tunasimamia na kudhibiti matumizi yake,” alisema.

Naibu Waziri huyo wa Fedha alisema eneo la tano ambalo litaangaliwa ni fedha ambazo hazitokani na kodi, bali zinachangwa na wananchi na wadau wengine katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
 
Alisema eneo hilo ni muhimu mbalo Serikali inaona kuna haja ya kulisimamia vizuri, ili kuhakikisha fedha za  wananchi zinatumika vizuri.

Jumanne, 10 Juni 2014

DKT. ASHA-ROSE MIGIRO ALIVYOPOKELEWA KWA FURAHA UMOJA WA MATAIFA


Ili kuwa ni hafla ya aina yake iliyojaa tabasamu, kukumbatiana na maneno ya " welcome back, good to see you again, we have missed you" yakitawala wakati Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha- Rose Migiro alipofika Ofisini kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon na kisha kukutana na kubadilishana mawazo na Katibu Mkuu mwenyewe wakianza na mazungumzo ya faragha kati yao wawili na kisha kujumuika na wafanyakazi wa Ofisi Binfasi ya Katibu Mkuu na Ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu. baada ya Mazungumzo yake na Katibu Mkuu, Dkt. Migiro pia alikutana na kufanya mazungumzo na Naibu Katibu Mkuu aliyemwachia kijiti Bw. Jan Eliasson.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akiwa na Dkt. Asha-Rose Migiro ( Mb) Naibu Katibu Mkuu Mstaafu na ambaye sasa ni Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati alipotembeleza Katibu Mkuu jana Jumatatu. Hii ni mara ya kwanza kwa Dkt. Migiro kufika Umoja wa Mataifa tangu alipostaafu Unaibu Katibu Mkuu miaka miwili iliyopita. Kabla ya Viongozi hao wawili kupiga picha hii rasmi, walikuwa na mazungumzo ya faragha ( Tete a tete). Waziri Migiro yupo hapa Umoja wa Mataifa kuhudhuria Mkutano ulioitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchango wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria katika Maendeleo Endelevu baada ya 2015.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon na timu yake akiwa katika mazungumzo na Dkt. Asha- Rose Migiro ambaye alifuatana na Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi. Katika mazungumzo hayo, Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa Waziri anayeshughulikia Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa. Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya Maofisa wake kwamba siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika Umoja wa Mataifa.
Ban Ki Moon akiagana na Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya mazungumzo yao.
Baada ya kuagana na Katibu Mkuu , Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dkt. Asha-Rose Migiro alielekea ofisini kwa Naibu Katibu Mkuu Bw. Jan Eliasson ambako nako kulikuwa na kukaribisha na tabasamu za akina yake. na kisha wakawa na mazungumzo ya faragha.Pichani ni Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson akimkaribisha kwa furaha Dkt. Asha- Rose Migiro ofisi kwake kwa mazungumzo.
Wakipata picha ya pamoja.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson akiwa na Dkt. Asha- Rose Migiro. Bw. Eliasson alimueleza Naibu Katibu Mkuu Mstaafu kwamba anajitahidi kufuata nyayo zake na kwamba anapenzi makubwa sana na Tanzania na Afrika kwa Ujumla, Bw. Eliasson aliwahi kufanya kazi Tanzania kama mwanadiplomasi chini ya Uongozi wa Rais wa wakati huo wa Sweden Marehemu Olof Palme.
Dkt. Asha- Rose Migiro akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson ( Leo jumanne ) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Dkt. Asha- Rose Migiro ( Mb) atakuwa miongoni wa wanajopo ( Panellist) watakaoendesha majadiliano kuhusu mchango wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika uungaji mkono juhudi za kitaifa na kimataifa katika kuutokomeza umaskini na maendeleo endelevu. Majadiliano hayo ni sehemu ya mkutano wa siku mbili ambao umeitishwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. John Ashe na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon.Kushoto ni Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu akipokea shada la Maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Ofisi Binafsi ya Katibu Mkuu. Ujio wa Dkt Migiro, uliamsha shamra shamra zaina yake kutoka kwa Katibu Mkuu mwenyewe ambaye kila wakati alikuwa akiachia tabasamu pana, Baraza lake la Mawaziri pamoja na wafanyakazi wa ofisi yake Binafsi pamoja na ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu.
" Hili UA zito ngoja tukupokee" ndivyo wanayoelekea kusema Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Mkuu wake wa Itifaki.
"welcome back" ndivyo anayosema afisa huyu wakati wakisalimia kwa furana ha Naibu Katibu Mkuu Mstaafu Dkt- Asha-Rose Migiro huku Katibu Mkuu akiangalia kwa furaha.
Ilikuwa ni furaha tupu kwa kweli salamu zikiendelea

uzinduzi wa maonyesho ya SIDO jijini Arusha


 Mkuu wa mkoa wa Arusha  Mhe Magessa Mulongo akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na kabila la Wahabeshi katika uzinduzi wa maonyesho ya  SIDO



baadhi ya bidhaa za shanga zilizopo katika maonyesho ya sido
 Mkurugenzi wa Taha Jacqueline Mkindi akiwa anaangalia na kufurahia bidhaa zinazotengenezwaa na shanga zilizopo katika viwanja vya makumbusho katika maonyesho ya wajasiriamali toka  viwanda vidogo vidogo
 wahazabe wakiendelea kutengenez mikuki yao

 Mkurugenzi wa SIDO Taifa Omary Bakari akiwa anasoma risala kwa mgeni rasmi katika maonyesho hayo


 Meneja wa Sido  Isidori kayenze Arusha akiendelea kunogesha maonyesho hayo

NSSF YAPIMA AFYA BURE KWA WAKAAZI WA MKOA GEITA


Kaimu Meneja wa Mafao ya Matibabu Dk. Lucy Simbila akizungumza kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Geita Dk. Ndinisyu Daniel (kushoto) kufungua zoezi hilo. Wengine ni Dr. Ali Mzige (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Bw.Shaban Mpendu, Meneja wa NSSF Mkoa wa Geita na Mwisho ni Regional Aids Control Cordinator (RACC), Elisande Shumbi.
wakazi wa Geita wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupima Afya zao.
Meneja wa NSSF GEITA, Bw. Shaban Mpendu akimsikiliza kwa makini  Dr. All MZIGE akimuelezea  mgeni rasmi kaimu mganga mkuu wa Geita   DR.Ndinsyu Daniel zoezi la upimaji sukari kwenye moja ya banda la upimaji afya.
Meneja NSSF Geita bwana Shaban Mpendu akimuongoza mgeni Rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Geita  DR. Ndinisyu Daniel kutembelea mabanda ya upimaji afya.
Afisa Mwandamizi  Uendeshaji   Bi.Siaeli akiandikisha wanachama wapya waliojitokeza kujiandikisha kwenye kambi ya upimaji Afya.
Mmoja ya watu waliojitolea kutoa damu kwa hiyari baada ya kupima Afya kwenye kambi hiyo ya upimaji Afya
Mmoja wa Madaktari akimpima mkazi wa Geita Urefu na Uzito ili kutambua uwiano wa urefu kwa uzito na kujua hali ya kiafya (BMI)

MWENYEKITI WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM (TAIFA) AWAAPISHA WANACHAMA 367 WAPYA WA CCM WILAYA YA NYASA MKOANI RUVUMA


 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo aliyevaa taji shingoni akicheza ngoma ya asili katika kijiji cha Kingirikiti Wilaya ya Nyasa wakati wa Ziara yake siku ya jana.
 Kikundi cha akina mama  kikitoa burudani
 Hata watoto nao wanavutiwa na mikutano ya Chama Cha Mapinduzi
 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo akitoa kadi kwa mwanachama mpya wa CCM kata ya LUMEME kijiji cha KINGIRIKITI wilaya ya Nyasa, kwa wanachama 367 waliojiunga na chama hicho cha CCM
 Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo akiwaapisha wanachama wapya wa  CCM
Wananchama wapya wa CCM wakiwa wamenyoosha kadi za Chama Cha Mapinduzi juu wakati wakiapa
Mwenyekiti  wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha mapinduzi CCM (Taifa) Bw. Abdallah  Bulembo akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya kuwaapisha wanachama wapya kijiji cha KINGIRIKITI kata ya LUMEME wilayani NYASA , Picha na kikosi cha Demashonews