Jumanne, 22 Aprili 2014

"Hatuna mpango wa kurudi Bungeni tena....Tutakachokifanya ni kuzunguka mikoani ili `kushitaki’ kwa wananchi"..UKAWA


 
LICHA ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta kuwa tayari kuzungumza na wajumbe wa Bunge hilo wanaounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wajumbe hao wametangaza kutokuwa tayari kurudi mjini Dodoma kwa majadiliano ya aina yoyote.
 
Badala yake, umoja huo umetangaza kuendelea na dhamira ya kuzunguka katika mikoa mbalimbali nchini ili `kushitaki’ kwa wananchi, kwa kile walichodai hawajaona mwelekeo wa kutetea na kusimamia maoni ya wananchi katika Rasimu ya Katiba mpya inayojadiliwa bungeni.
 
Hayo yalisemwa jana mjini Zanzbar na viongozi wa Umoja huo, Freeman Mbowe na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye Hoteli ya Mazson iliyopo Shangani.
 
Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, alisema kwa sasa wanajiandaa kwenda kwa wananchi, kuelezea na kutetea msimamo wa serikali tatu.
 
“Msimamo wa UKAWA ni kwamba haturudi tena katika Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu tumeona kwamba wenzetu wa chama tawala, hawapo tayari kujadili Katiba kwa njia za kistaarabu na badala yake matusi yametawala ikiwemo ubaguzi,” alisema Mbowe.
 
Alisema wamejipanga kuzunguka nchi nzima ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuelezea maoni ya wananchi kuhusu Katiba ambayo ni msimamo wa serikali tatu, kwa mujibu wa maoni ya Tume ya Kurekebisha Katiba, iliyokuwa chini ya Jaji mstaafu Joseph Warioba.
 
Mbowe alisema masikitiko yao makubwa ni kwamba maoni hayo, yanapingwa katika Bunge Maalumu la Katiba na chama tawala cha CCM, chenye idadi kubwa ya wajumbe katika Bunge hilo Maalumu.
 
“Msimamo wa maoni yaliyotolewa na wananchi tangu awali ni serikali tatu kwa mujibu wa Tume ya Jaji Warioba...lakini kwa bahati mbaya maoni hayo yanapingwa na wenzetu wa CCM,” alisema Mbowe.
 
Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyegombea urais mfululizo tangu mwaka 1995, baada ya kurudishwa kwa mfumo wa vyama vingi, akizungumza, alisema wanatarajia kufanya mkutano mwingine mara baada ya kumalizika kwa Sikukuu ya Pasaka.
 
Alisema wamekubaliana na maombi, yaliyotolewa na Jeshi la Polisi ya kutoa nafasi kwa wananchi kusherehekea Sikukuu ya Pasaka kwa utulivu.
 
“Hatuondoki Zanzibar hadi tufanye mkutano wetu, wenye lengo la kuwajulisha wananchi kinachofanyika Dodoma katika Bunge la Katiba ambacho ni kinyume na maoni yao,” alisema Lipumba.
 
Jeshi la Polisi Zanzibar limezuia mkutano, uliokuwa ufanywe na Umoja huo, unaoundwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa na wafuasi wao walioko katika Bunge Maalumu la Katiba.
 
Hata hivyo, Jeshi hilo halikuzuia Ukawa pekee kufanya mkutano, bali hata mikutano mingine ukiwemo uliokuwa ufanywe na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), nao ulizuiwa.
 
Ukawa, baada ya kususia Bunge katikati ya wiki hii, walipanga kuzungumza nchi nzima kuelezea kile wanachodai kuonewa na `kubanwa’ katika mijadala ya vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, vinavyoendelea mjini Dodoma.


TASWIRA KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO


Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) akibadlishana mawazo Mjumbe wa Bunge hilo Rashid Mtuta (kushoto) leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi.

Naibu Katibu wa Bunge Maalum ambaye ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Thomas Kashillah (mwenye miwani) akibadlishana mawazo na Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuendelea na mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Profesa Costa Mahalu (kushoto) na Profesa Mark Mwandosya (kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuanza mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiwasili kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili kuendesha na kusimamia mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiongoza dua ya kuliombea Bunge na Taifa kabla ya kuanza mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati wa mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakishiriki dua ya kuliombea Bunge hilo leo mjini Dodoma kabla ya kuanza mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya. picha na Bunge Maalum la Katiba-Dodoma.

TASWIRA ZA AJALI YA BASI LA LUHUYE LILILOUA ZAIDI YA WATU 10 JANA MKOANI MWANZA




Basi la abiria la Luhuye Express lenye namba za usajili T 410 AWQ baada ya kuacha njia na kugonga nyumba katika Kijiji cha Yitwimila 'A', wilayani Busega, Mkoa wa Simiyu jana asubuhi.


Wananchi wakishuhudia ajali hiyo iliyoua watu zaidi ya 10 na kujeruhi 30.

Basi la abiria la Luhuye Express baada ya kupinduka.

Baadhi ya majeruhi katika ajali hiyo mbaya.
AJALI hii mbaya iliyopotea uhai wa watu zaidi ya 10 na kujeruhi 30 ilitokea jana katika Kijiji cha Yitwimila 'A', Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu majira ya saa 4 asubuhi.

SINTAH BANA KWA KUJICHETUA ETI LEO HII ANAMKUBALI WEMA SEPETU WAKATI ALIWAHI KUTAMKA KUWA HAMPENDI KAMA NINI KUMBE MNAFIKI TU:


Mmmh makubwa ya wakubwa waliompigia kura ndio hao wanamchambua huko insta, yaani Instagram ni ya kiswahili sana, nasubiri siku niamke nikute imefungwa, maana majority hawana kazi ya kufanya zaidi ya kufungua fake accounts na kutukana, wakiamka asubuhi before kupiga mswaki wanapitia pics za watu ili wajue cha kuwatukana hivi unafaidika nini yarabi?? kujiita Team mavimavi na Team ujinga, like pic n comment where necessary usipojisikia kausha sasa matusi ya nini
hilo shindano lilikuwa wazi, wanaadam ndio wamepiga kura sasa kama kashinda kuna ubaya? after all katika mashindano lazima atokee mshindi tupende tusipende, waandaji walitoa nafasi kwa wasomaji kuchagua wanaomuona bora na wakamchagua sasa ubaya wa nini kumnanga ooh hakustahili nyie si ndio wapiga kura sasa makelele ya nini khaaaa
katika hilo shindano Wema alikuwa anashindana na Wolper,Lulu,Nelly,Jokate na Wema kuibuka mshindi
 mie ndio mtazamo wangu je wewe??

HIVI NDIVYO WEMA ALIVYOKUFA NA KUOZA KWA DIAMOND PLATNUMZ, HAONI WALA KUSIKIA...CHEKI HAPA


Mapenzi Ni Kitu cha ajabu sana kiasi cha kufikia hata kumfanya mtu kuwa kama chizi au mwehu na kukubaliana na hali yoyote ilimradi apate tu PENZI. Hii imethibitika zaidi jana Baada ya Madame Wema Sepetu Kutupia picha mtandaoni akiwa na mpenzi wake Diamond Platnumz huku Diamond akiwa amechora tatoo yenye jina la mwanamke mwingine tofauti kabisa na Wema, kama unavyoona hapo kwenye picha mkononi inasomeka "SANDRA". 
Bila shaka tutafanya uchunguzi wa kina na kukuletea majibu kamili kuhusiana na Mwanamke huyu Sandra ambaye bado Diamond anamficha.

Rais Kikwete amtumia salamu Waziri Mkuu kuomboleza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa, Ndugu Moshi Chang’a.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuomboleza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mkoa wa Rukwa, Ndugu Moshi Chang’a.

“Ni kifo cha kusikitisha kwa sababu kimepunguza safu ya uongozi wetu na kimelinyang’anya taifa letu mhamasishaji hodari na mtetezi wa kuaminika wa maendeleo ya wananchi,” Rais Kikwete amesema katika salamu hizo.

Amesema Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi: “Nilimjua Ndugu Chang’a kwa miaka mingi tokea mwaka 1979 alipojiunga na utumishi wa Chama cha Mapinduzi ambacho pia alikitumia kwa uaminifu mkubwa hadi alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya mwaka 2003. Alikuwa kiongozi wa kweli kweli wa maendeleo na kifo chake kimetuachia pengo la uongozi.”

“Nakutumia salamu zangu za dhati kuomboleza msiba huu. Aidha, kupitia kwako, naitumia familia wa Ndugu Chang’a pole za dhati ya moyo wangu kwa kuondokewa na mzazi na mhimili wa familia. Nakuomba uwajulishe kuwa naelewa machungu yao katika kipindi hiki na nawaombea subira na uvumilivu kwa sababu yote ni mapenzi ya Mungu. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya marehemu. Amen,” amesema Rais katika salamu hizo.

Ndugu Moshi Chang’a ambaye aliaga dunia jioni ya jana, Jumapili, Aprili 20, 2014  katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, Dar Es Salaam amekuwa mkuu wa wilaya katika Mikoa ya Mbeya, Tabora na Rukwa.
Imetolewa na;
 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014

Alhamisi, 17 Aprili 2014

KIOJA KANISA LA GWAJIMA ,MAITI YAOMBEWA IFUFUKE, YAGOMA



Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege wakipeleka mwili wa ndugu yao kanisani kwa ajili ya maombi.

Haruni Sanchawa na Gabriel Ng’osha
HIKI ni kioja! Ndugu wa marehemu Elitha Kaizilege ambaye alipatwa na mauti katika Hospitali ya Kairuki iliyopo Mikocheni jijini Dar wiki iliyopita, walifanya tukio la aina yake baada kutokukubali kama ndugu yao amefariki.Ndugu hao wa marehemu walizuia mwili huo kupelekwa mochwari na badala yake wakauombea kwa saa sita hospitalini hapo wakiamini ataamka, kwani ugonjwa wake ni wa kulogwa.
Kana kwamba haitoshi, baada ya muda huo kupita, ndugu hao, wanaosadikika kuwa ni waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima, waliupeleka kanisani hapo ambapo uliombewa zaidi ya saa mbili mwili huo ili uamke, ikashindikana.

Mchungaji Gwajima akiwa kazini.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, marehemu ambaye alirejea nchini hivi karibuni kutoka Marekani alikoenda kuhudhuria mahafali ya mwanaye anayesoma nchini humo, alianza kuumwa kimasihara, hasa kwa vile ugonjwa wake ulikuwa haueleweki licha ya kupelekwa katika hospitali mbalimbali jijini.
Wakati akiumwa, inadaiwa kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni sikio lakini katika vipimo kadhaa alivyopimwa, havikuonyesha ugonjwa.
Kwa mara ya mwisho kuna madai kuwa alikuwa na kansa ya kichwa, kitu ambacho pia kiliwashangaza ndugu ambao walishangaa ni wapi alipoutoa ugonjwa huo mara moja.

Mchungaji Gwajima katika harakati ya kumtoa mapepo mgonjwa.
Inadaiwa pia kuwa wakati akiumwa, mama huyo aliwahi kupigiwa simu na mtu anayehisiwa ni mganga wa kienyeji kutoka Kigoma, ambaye haikufahamika walichoongea.
Inasemekana kuwa mara tu baada ya madaktari wa Hospitali ya Kairuki kuwataarifu kuhusu kifo cha mgonjwa wao, walizuia mwili huo kupelekwa chumba cha maiti wakiamini hajafariki, na kwamba wanataka wafanye maombi ili kumfufua.

Baada ya maombi ya hospitalini na kanisani kushindikana, mchungaji aliyeongoza ibada hiyo, ambaye jina lake halikuweza kujulikana mara moja, aliwaambia ndugu hao kuwa marehemu hataweza kuamka na kuwataka waupeleke mwili huo chumba cha kuhifadhia maiti.
Waandishi wetu walimtafuta kiongozi mkuu wa kanisa hilo mchungaji Josephat Gwajima ili aweze kuzungumzia suala hilo, lakini waliambiwa kuwa yuko Japan kwa kazi ya kuhubiri neno.
Hata hivyo, mmoja wa viongozi waandamizi wa kanisa hilo, aliyekataa jina lake kutajwa gazetini, alisema maombi ya aina hiyo hufanyika kanisani hapo na mara kadhaa, watu waliodhaniwa wamefariki waliweza kuinuka.

DIAMOND AINGIA KWENYE NOMINATION CATEGORY MBILI MTV AFRICA MUSIC AWARDS

Thursday, 17 April 2014


Nomination za MTV Africa music awards kwa mwaka 2014 zimetoka huku Mafikizolo,Uhuru na Davido wakiongoza kwa kupata nomination 4.
Watanzania wapo kwenye vipengele vitatu na moja ya vipengele hivyo vinasubiliwa kwa hamu kumjua mshindi kwasababu ni moja ya vipengele vikubwa kwenye awards hizo.
Best Male
Anselmo Ralph (Angola)
Davido (Nigeria)
“Diamond (Tanzania)“
Donald (South Africa)
Wizkid (Nigeria)
Best Female
Arielle T (Gabon)
Chidinma (Nigeria)
DJ C’ndo (South Africa)
Efya (Ghana)
Tiwa Savage (Nigeria)
Best Group
Big Nuz (South Africa)
Mafikizolo (South Africa)
Mi Casa (South Africa)
P Square (Nigeria)
Sauti Sol (Kenya)
Best New Act
Burna Boy (Nigeria)
Heavy K (South Africa)
Phyno (Nigeria)
Stanley Enow (Cameroon)
Uhuru (South Africa)
Best Live Act
2face (Nigeria)
Fally Ipupa (DRC)
Flavour (Nigeria)
Dr Malinga (South Africa)
Zakes Bantwini (South Africa)
Best Collaboration
Amani ft Radio and Weasel – ‘Kiboko Changu’ (Kenya/Uganda)
“Diamond feat Davido – ‘Number One’ (Remix) (Tanzania/Nigeria)“
Mafikizolo feat May D – ‘Happiness’ (South Africa/Nigeria)
R2bees feat Wizkid – ‘Slow Down’ (Ghana/Nigeria)
Uhuru feat DJ Buckz, Oskido, Professor, Yuri Da Cunha – ‘Y-tjukutja’ (South Africa/Angola)
Artist of the Year
Davido (Nigeria)
Mafikizolo (South Africa)
Mi Casa (South Africa)
P Square (Nigeria)
Uhuru (South Africa)
Song of the Year
Davido- ‘Skelewu’ (Nigeria)
DJ Clock feat Beatenberg – ‘Pluto’ (Remember Me) (South Africa)
DJ Ganyani feat FB – ‘Xigubu’ (South Africa)
DJ Kent feat The Arrows –‘Spin My World Around’ (South Africa)
Dr Sid feat Don Jazzy – ‘Surulere’ (Nigeria)
KCee – ‘Limpopo’ (Nigeria)
Mafikizolo feat Uhuru ‘Khona’ (South Africa)
Mi Casa- ‘Jika’ (South Africa)
P Square – ‘Personally’ (Nigeria)
Yuri Da Cunha -‘Atchu Tchu Tcha’ (Angola)
Best Hip Hop
AKA (South Africa)
Ice Prince (Nigeria)
Khuli Chana (South Africa)
Olamide (Nigeria)
Sarkodie (Ghana)
Best Pop
Danny K (South Africa)
Fuse ODG (Ghana)
Goldfish (South Africa)
LCNVL (South Africa)
Mathew Mole (South Africa)
Best Alternative
Gangs of Ballet (South Africa)
Michael Loman (South Africa)
Nakhane Toure (South Africa)
Parlotones (South Africa)
Shortstraw (South Africa)
Best Francophone
Arielle T (Gabon)
Espoir 2000 (Ivory Coast)
Ferre Gola (DRC)
Toofan (Togo)
Youssoupha (Congo)
Best Lusophone
Anselmo Ralph (Angola)
JD (Angola)
Lizha James (Mozambique)
Nelson Freitas (Cape Verde)
Yuri Da Cunha (Angola)
NON MUSIC CATEGORIES
Personality of the Year
Chimamanda Adiche (Nigeria)
Omotola Jalade Ekeinde (Nigeria)
Trevor Noah (South Africa)
Lupita Nyong’o (Kenya)
Yaya Toure (Cote d’Ivoire)
Transform Today by Absolut
Anisa Mpungwe (Tanzania)
Clarence Peters (Nigeria)
I See a Different You (South Africa)
Leti Arts (Ghana)
Rasty (South Africa)
Unaweza kuanza kupiga kura kupitia  www.mtvbase.com mwisho wa kupiga kura ni 4 June 2014.

TAZAMA PICHA,LULU AKIWA NA BIBI YAKE UONE WALIVYOFANANA

Thursday, 17 April 2014



LULU MICHAEL NA BIBI YAKE
Mwigizaji maarufu na wa filamu na maigizo ya kibongo Lulu amepiga picha hiyo na bibi yake  mzaa mama baada ya  bibi huyo kuja dar es salaam kumtembelea mwanae {mama wa lulu} na wajukuu zake.
Eti wanafanana toa maoni yako hapo chini

 
Credit: Bongoclan

HAWA NDIO MASTAA 20 WENYE USHAWISHI ZAIDI NCHINI TANZANIA. WEMA ASHIKA NAMBA 1. SOMA HAPA

Thursday, 17 April 2014


Wakati mwingine si kitu rahisi kupima ushawishi lakini tutaangalia ni wazo mawazo gani ya mtu, mifano gani ya mtu, kipaji gani cha mtu na ugunduzi gani wa mtu uliobadilisha jambo katika nchi yetu. Hawa ndio mastaa 20 wa burudani, michezo na urembo Tanzania wenye ushawishi mkubwa zaidi 1. Wema Sepetu Well, well, well kunaweza kukawa na mjadala mrefu sana hapa wa kwanini mrembo huyu akamate nafasi ya kwanza wakati kila kukicha amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa scandals kibao. Hiyo ni kweli lakini ukiugeuza umaarufu huo wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa biashara na jinsi anavyokubalika, hakuna anayemfikia Wema. Wema ni brand inayouzika kirahisi. Kuandikwa mara kwa mara kwenye magazeti ya udaku ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule unayemjua hapa Tanzania. Iwe picha akiwa kwa daktari aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa nywele, tattoo aliyojichora, picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha zinamuonesha akiwa na shoga zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu Wema kinavutia attention ya watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata comments nyingi kuliko za wengine wote. Kama leo hii Wema akisema aanzishe bidhaa yoyote inayowalenga vijana, haitachukua muda kushika na kutafutwa kama njugu. Wema ni show stopper! Kama akiingia ukumbini kwenye shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda kutokana na watu kugeuka kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati akielekea sehemu ya kukaa. Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa muigizaji wa orodha A Tanzania, CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame Films, Wema Sepetu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa. Ni msanii gani Tanzania ambaye nyimbo zake zinahit mtaani bila hata kupigwa redioni? Bila shaka umeshasikia nyimbo nyingi za Diamond mtaani siku za hivi karibuni ukiwemo UKIMWONA na ukajiuliza iweje unahit wakati haujaachiwa rasmi? Muziki wa Diamond umekuwa ukitumika kama tulizo la wanyonge walio kwenye mahaba mazito. Kuanzia Mbagala, Nitarejea, Lala Salama, Mawazo ama Nataka Kulewa, zote zimekuwa zikitumiwa na watu wa rika mbalimbali, madaraja tofauti ya kiuchumi, wanawake kwa wanaume na watoto kama burudisho la roho zao. Diamond Platnumz hi hitmaker na haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Diamond ndiye msanii anayefanya show nyingi zaidi ndani na nje ya Tanzania na kwa kulipwa gharama kubwa kuliko msanii mwingine yeyote muda huu. Hujaza kumbi kubwa za starehe yeye mwenyewe bila backup ya msanii mwingine na kuwaacha wasichana wakibubujikwa na machozi ya furaha na kutamani walau kukishika tu kifua chake kilichoanza kupasuka kwa mazoezi. Kwa mujibu wa kampuni ya Push Mobile, Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasib ndiye msanii anayeuza zaidi nyimbo zake kama miito ya simu (RBT). Pamoja na kuzungukwa na scandal kibao kuhusu wanawake, Diamond ni kijana mwenye mawazo pevu na ya kiutuuzima. Akiwa ametoka kwenye familia duni na kupata misukosuko mingi ikiwemo kutengwa na baba yake na kulelewa zaidi na mama yake, Diamond amekuwa akitoa ushauri na kuwapa moyo watafutaji wa maisha wasikate tamaa. Hupenda kutoa ushauri kwa vijana wenzie kuhusiana na umuhimu wa kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu mwenyezi Mungu na kutokata tamaa. Katika kuhakikisha kuwa anaitolea pia jamii, hivi karibuni alitangaza kuwa na nia ya kujenga msikiti. Ni kwa sababu zipi kijana huyu asiwe na ushawishi?
Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP. Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 40,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 90,000. Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki. Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.
Nancy Sumari ni msichana mrembo, mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania wa kwanza aliyewahi kufika mbali zaidi kwenye shindano la Miss World ambapo mwaka 2005 alifanikiwa kuwa Miss World Africa. Kwa sasa Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anasoma Shahada ya Biashara. Pia ni mjasiriamali na anafanya kazi zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha watoto wa kike kujitambua na kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao. Katika harakati zake za kuhakikisha wasichana wa Tanzania wanatambua haki zao, anaendesha programu iitwayo Mentorship, ambayo inazunguka kwenye shule mbalimbali za serikali za wasichana nchini, na kuzungumza nao kuhusu maisha. “Kwenye programu hiyo, tunabadilishana mawazo na wanafunzi na wao wanazungumza changamoto wanazokutana nazo na kupeana mawazo jinsi ya kufanya kwani nawaambia wakiamua kuthubutu wanaweza kufanikiwa, na wanaonesha wanaweza,”Nancy aliliambia gazeti la Habari Leo hivi karibuni. Pamoja na hayo pia Nancy anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwenye kampeni ya kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za sekondari za serikali nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu. Hivi karibuni alizindua kitabu chake kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’ kinachomlenga mtoto wa kike kuona jinsi wanawake wengine walivyofanikiwa licha ya kupitia changamoto mbalimbali. “Ninaamini kitabu kitasomwa na wengi ndio maana nikaamua ujumbe wangu niufikishe kwa njia hii, watasoma watoto wetu hata wajukuu kitajenga kitu kwenye akili ya mtoto na wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao watathubutu” aliliambia Habari Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa kutoka kwa mrembo huyu

MJINI KUNA MAMBO,ETI MSANII JUX ASADIKIKA KUWA FREEMASONRY~ USHAHID HUU HAPA

Thursday, 17 April 2014



Karne hii watu maarufu wamekuwa wakijiweka wazi kukiri kujiunga katika jumuiya ya watu wanaomwabudu shetani "Freemason" kama Jay z, Kanye West, Drake, Lady Gaga na wengine kibao kwa minajili ya kujipatia utajiri na umaarufu na ndipo hata siri zao zimekuwa
zikivuja siku hadi siku. Mingoni mwa siri zao hizo ni nembo ambazo zimekuwa zikiwawakilisha zikiwa na maana ya kumpinga Mungu na kumpa sifa shetani. 
Msalaba uliogezwa ""Inverted Cross" ni moja kati ya nembo hizo ukiwa na maana ya kwenda kinyume na ukristu unaomtukuza Mungu. Juma Jux katika video yake mpya ya Nitasubiri anaeyoendelea kushoot huko China ameonekana akiwa ametupia vazi lenye msalaba uliogeuzwa.
 Juhudi zinaendelea kupata mawasiliano nae ili kujua ukweli
wa jambo hili kama anajua chochote kuhusu hili au yeye kwake hizo ni swagz tu.

Credit..... hotnewsdaily

TAZAMA PICHA ZA VAZI JIPYA LILILOBUNIWA NA MBUNIFU WA MAVAZI,MTANZANIA MISSY TEMEKE



MISSY TEMEKE
Missy Temeke  wa kwetu fashion,siyo jina geni kwenye tasnia ya urembo na
fashion.ni Mwanadada mrembo aishie nchini Marekani
anayejihusisha zaidi na ubunifu wa  mavazi yenye mwonekano wa
kitanzania na kiafrika chini ya label yake ya KWETU FASHION.
.ametoa collection mpya ya vazi Lenye mwonekano wa kiafrica..
SOURCE


MAMODO WA KWETU FASHION WAKIONYESHA
VAZI ALILOBUNI ,MISSY TEMEKE




MVUA ZAHARIBU RELI YA DSM-TANGA-MOSHI.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgLlzfwEIfm5pGwu1K_jx5iz_Y_WP0TnA2LaTA_JarLJDzTVDJDJIcZODbtZ6s1x80uqZHrgBnaeA769ImXrfjJ8N5sDmgdEcU22HcGu5AYrtMaFOFDDcsGOZuLkETwGyMt3KiPxi7W9q_3/s1600/DSC_0446.JPGSehemu ya njia ya reli katika eneo la Ming’ongo ikiwa inaning’inia baada ya tutakusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipalo Amani Kisamfu pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona athari kubwa iliyotokea kwenye njia ya reli. Aidha, katika njia hiyo kilomita kumi na nane za njia ya reli zimeaharibiwa na mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhAf8UB_jUvi_8GMS9uyJHj2EKxQdsafYguk3VHKYzzBu9d3UlN_dDE2ixbraj8DcICyjDp83pw_ihsMUMSn_ARx7IeBi9LA3492rFMJmrY72Rz8sNYqoYPLbfMgxQZeZuqxZ2_hIMpG0b6/s1600/DSC_0439.JPGMkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Reli, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Festo Mwanjika (wa pili kutoka kulia) akiangalia uharibifu mkubwa uliotokea kwenye njia ya reli katika eneo la Ming’ong’o kilomita 4 kutoka Stesheni ya Ruvu, alipotembelea eneo hilo kujionea moja kati ya sehemu kumi na nane zilizoharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Uchukuzi)

EXCLUSIVE:YANI KAMA HAUJAJIUNGA INSTAGRAM UNAKOSA UHONDO KINOMA,TAZAMA HAMISA MOBETO NA YEYE AAMUUA KUPOST PICHA ZA UTATA, YANI NI FULL SHIDAH KWA VIDUME VYA MBEGU




Mwanadada Hamisa Mobeto amejikuta akipost picha hizi katika mtandao wa  Instagram baada ya kuonyesha mapenzi ya dhati kwa huyu model,


 zicheki picha zenyewe hapo chini






BINTI WA KIBONGO MWANA CHUO ASABABISHA MZUNGU KUFUKUZWA KAZI

Raia mmoja wa nchini Finland amejikuta katika wakati mgumu sana baada ya kushindwa kufanya lolote kazini alipoajiriwa baada ya kutaka kuwa katika mahusiano na mwanadada huyu wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye alimteka akili kiasi cha kumfanya Mzungu huyo kuwa anashinda chuoni kutwa nzima kubembeleza akubaliwe jambo lililomsababishia aache kuhudhuria kazini kwa muda wa miezi mine mfululizo kutokana na kupagawishwa na uzuri wa mwanadada huyu ambao umemfanya awe gumzo chuo kizima. Mzungu huyo  ambaye ni muajiriwa wa kampuni moja ya simu za mkononi (Jina limehifadhiwa) hapa jijini alikuja Tanzania mwaka jana kwa dhumuni la kufanya kazi kwa mkataba amejitia matatizoni baada ya kumtaka kimapenzi mrembo huyu ambaye alikutananae kwa mara ya kwanza katika coffe bar moja iliyopo Mlimani city na kwakushindwa kuzuia hisia zake alijikuta akiomba mawasiliano ya mrembo huyu jambo ambalo ndio hasa limemsababishia matatizo kutokana na ukweli kwamba Mzungu huyo amekuwa akimbembeleza sana mrembo huyu bila mafanikio  kiasi cha kumfanya aweanashinda Chuoni kwa huyu dada huyu Mlimani main campas. 

Utoro sugu wa Mzungu huyo umemuweka katika wakati mgumu kwani amepewa barua mbili za onyo mpaka sasa na amebakiza barua ya mwisho aachishwe kazi jambo ambalo mwenyewe anasema kuwa yuko katika wakati mgumu sana kwani hayuko tayari kumkosa dada huyo licha ya ukweli kwamba nchini kwao ameacha mke na watoto. 
Nilipomfanyia mahojiano dada huyo alidai hawezi kuwa na mtu ambaye hana m,alengo nae ya muda mrefu kwani uwepo wake hapa nchini ni wa muda mfupi tu hivyo yeye hayuko tayari kuwa kama chombo cha starehe kwa kila mpita njia. Licha ya kumpongeza dada huyo nilitaka nifahamu kama ameshamwambia ukweli Mzungu huyo ambapo dada alieleza kuwa ukweli ameshamwambia lakini jamaa huyo amekuwa king’ang’anizi kiasi cha kumnyima mpaka muda wa kujisomea jambo linalomfanya akate shauri la kwenda kumripoti katika kituo cha polisi kilichopo chuoni hapo endapo kesho siku ya kesho atathubutu kumfata tena

MAKALIO YA MWALIMU WA SEKONDARI YASABAISHA WANAFUNZI WA KIUME KUSHINDWA KUSOMA WAZAZI WAOMBA AONDOLEWE ILI KUWANUSURU WANAFUNZI HAO



Mtandao huu umetumiwa picha hii ya mwalimu wa shule moja ya Sekondari iliyopo Mkoani Kagera vijijini ambae amelalamikiwa na wazazi kufuatia wanafunzi wa shule hiyo kushindwa kusoma vizuri kisa makalio yake makubwa ambayo kipindi akiwa anaandika somo ubaona huku nyuma yakitikisika kwa staili ya kipekee.
Kwa mujibu wa mzazi huyo ambae alimvizia dada huyo akiwa kwenye nyumba za walimu na kumpiga picha inayoonekana hapo juu alisema" Unajuwa huyu mwalimu anafundisha kidato cha kwanza huku ifahamike wanafunzi wengi wa umri huo ni wale wanaobarehe hivyo inawauwiya vugumu kuvumilia shughuri aliyonayo mwalimu huyo nyuma" Alisema mzazi huyo ambae aliomba hifadhi ya jina lake

INASIKITISHA ,MWANAMKE AGONGWA NA DALADALA URAFIKI JIJINI DAR ES SALAAM.



MWANAMKE mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja akiwa ni mkazi wa Dar leo asubuhi aligongwa na gari aina ya Toyota Coaster inayofanya shughuli za daladala kwenye barabara za Morogoro jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilitokea eneo la Urafiki jijini Dar es Salaam. Walioshuhudia tukio walisema majeruhi huyo alikuwa katikati ya barabara mbili akitaka kuvuka kuelekea eneo la kituo cha polisi cha Urafiki lakini bahati mbaya aliyumba na kudondokea daladala hiyo iliyokuwa nyuma yake ambayo ilimburuza kwenye ukingo wa barabara hiyo.Picha mbalimbali zikionesha Wasamaria wema wanavyomuokoa majeruhi huyo.
 
PICHA NA: RICHARD BUKOS / GPL