Mwenyekiti
wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi
amewasili leo Alhamis tarehe 10-4-2014 saa nne asubuhi katika Uwanja wa
ndege wa Bukoba Mjini na kupokelewa na Wadau wengi, Huku ikiwa ni mara
ya kwanza tangu achaguliwe Rais wa TFF.
Bw.
Jamal Malinzi baada ya kutua amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa
Kagera na baadae kuhudhulia Kikao cha kamati Tendaji ya KRFA na siku
inayofuata utakuwepo mkutano mkuu wa KRFA.
Kulia
ni Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA ,
Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao
makuu, nae alikuwepo Uwanja wa Ndege Bukoba kwa mapokezi ya Rais wa TFF
Ndugu Jamal Malinzi. Na hapa wakiteta jambo kwa kushirikishana na wadau
pamoja na Viongozi.
Rais
wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi (kulia)
akizungungumza na baadhi ya Viongozi wa Soka na wadau waliojitokeza
kumpokea leo kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo. Kushoto ni Bw.
Salum Chama Katibu wa KRFA Kagera, Anayefuata ni Bw. Ndg Ruge Masabala
Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi
Kushoto
ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil
Malinzi kwenye picha na Mwandishi wa Mtandao wa Jamii Bukobasports.com
leo muda mchache alipotua kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo.
Kwa
furaha tele..Bw. Al-amin Abdul Abdul baada ya kumuona Kiongozi, Rais wa
TFF leo hii kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe Rais wa TFF.
Karibu Mkuu, Bw. Al-amin Abdul Abdul akimkarisha nyumbani Bukoba Bwana Jamal Malinzi
Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga (kulia) akisalimiana na Al-amin
Bw. Willy O. Rutta, (Willy Kiroyera) nae alikuwepo uwanjani hapo kumpokea Rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi.
Picha ya pamoja ilipigwa
Siku nyingi sana!!
Karibu Mkuu, Willy Kiroyera akimkaribisha Rais wa TFF
Hapa ndio Bukoba Mkuu, Mambo yamebadilika kwa muda mfupi tuu!
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi akishuka
kwenye gari kwenye Hotel aliyofikia ya Victoria Perch.
Karibu sana..
Wadau wa Soka Mkoani Kagera
Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga akizungumzia swala zima la mkutano mkuu wa KRFA utakao fanyika hivi karibuni.
Bw. Willy O. Rutta
0 maoni:
Chapisha Maoni