Ijumaa, 11 Aprili 2014

Lulu Michael alia na watu wanaotumia jina lake Facebook kuchangisha fedha....Watu hao wamepost video za ngono facebook kwa jina lake



Muigizaji wa bongo movies Elizabeth ‘Lulu’ Michael ameelendelea kuwa mmoja kati ya waathirika wa vitendo vinavyofanywa na watu wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kwa majina ya watu maarufu kwa lengo la kujipatia fedha.

 Watu hao ambao wanafungua akaunti mbalimbali kwenye Facebook kwa jina la Elizabeth Michael wamepost maelezo yanayoonesha kuwa muigizaji huyo ameendelea kuchangisha fedha kwa ajili   ya mfuko wa marehemu Steven Kanumba kwa madai kuwa anasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kutaja kiwango ambacho ameshakipata huku akiomba watu waendelee na moyo huo.
Akaunti feki ya Lulu katika mtandao wa kijamii wa Instagram. 
 
Muigizaji huyo ameandika kwenye Instagram kuwatahadhalisha watu dhidi ya matapeli hao ambao wamepost video ya ngono kwenye ukurasa huo ikionesha kuwa yeye ndiye kafanya hivyo. 
 
“Dah sijui niseme vipi…hizi facebook accounts sio zangu…kama huyu anaomba michango eti…dah the same account ipe post video ya ex…..na ziko account nyingi sana….now mm sina account yoyote facebook nina fan page moja tu ELIZABETH LULU MICHAEL….kwahiyo kuweni makini na hao matapeli…na nyie mnaotumia jina langu vibaya I thnk it[s time to leave me alone…kwa hayo mapenzi ya kutumia jina langu ovyo nimeshindwa mm…..”Ameandika  Lulu Michael

0 maoni:

Chapisha Maoni