Home »
» HAWA NDIO MASTAA 20 WENYE USHAWISHI ZAIDI NCHINI TANZANIA. WEMA ASHIKA NAMBA 1. SOMA HAPA
Wakati mwingine si kitu rahisi kupima ushawishi lakini tutaangalia ni
wazo mawazo gani ya mtu, mifano gani ya mtu, kipaji gani cha mtu na
ugunduzi gani wa mtu uliobadilisha jambo katika nchi yetu. Hawa ndio
mastaa 20 wa burudani, michezo na urembo Tanzania wenye ushawishi mkubwa
zaidi
1. Wema Sepetu
Well, well, well kunaweza kukawa na mjadala mrefu sana hapa wa kwanini
mrembo huyu akamate nafasi ya kwanza wakati kila kukicha amekuwa
akigonga vichwa vya habari kwa scandals kibao. Hiyo ni kweli lakini
ukiugeuza umaarufu huo wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa biashara
na jinsi anavyokubalika, hakuna anayemfikia Wema. Wema ni brand
inayouzika kirahisi. Kuandikwa mara kwa mara kwenye magazeti ya udaku
ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu
inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa
zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule
unayemjua hapa Tanzania.
Iwe picha akiwa kwa daktari aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa
nywele, tattoo aliyojichora, picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha
zinamuonesha akiwa na shoga zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu
Wema kinavutia attention ya watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata
comments nyingi kuliko za wengine wote.
Kama leo hii Wema akisema aanzishe bidhaa yoyote inayowalenga vijana,
haitachukua muda kushika na kutafutwa kama njugu. Wema ni show stopper!
Kama akiingia ukumbini kwenye shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda
kutokana na watu kugeuka kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati
akielekea sehemu ya kukaa. Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa
muigizaji wa orodha A Tanzania, CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame
Films, Wema Sepetu ni mwanamke mwenye ushawishi mkubwa.
Ni msanii gani Tanzania ambaye nyimbo zake zinahit mtaani bila hata
kupigwa redioni? Bila shaka umeshasikia nyimbo nyingi za Diamond mtaani
siku za hivi karibuni ukiwemo UKIMWONA na ukajiuliza iweje unahit wakati
haujaachiwa rasmi? Muziki wa Diamond umekuwa ukitumika kama tulizo la
wanyonge walio kwenye mahaba mazito. Kuanzia Mbagala, Nitarejea, Lala
Salama, Mawazo ama Nataka Kulewa, zote zimekuwa zikitumiwa na watu wa
rika mbalimbali, madaraja tofauti ya kiuchumi, wanawake kwa wanaume na
watoto kama burudisho la roho zao. Diamond Platnumz hi hitmaker na
haoneshi dalili za kupunguza kasi.
Diamond ndiye msanii anayefanya show nyingi zaidi ndani na nje ya
Tanzania na kwa kulipwa gharama kubwa kuliko msanii mwingine yeyote muda
huu. Hujaza kumbi kubwa za starehe yeye mwenyewe bila backup ya msanii
mwingine na kuwaacha wasichana wakibubujikwa na machozi ya furaha na
kutamani walau kukishika tu kifua chake kilichoanza kupasuka kwa
mazoezi.
Kwa mujibu wa kampuni ya Push Mobile, Diamond ambaye jina lake halisi ni
Nasib ndiye msanii anayeuza zaidi nyimbo zake kama miito ya simu (RBT).
Pamoja na kuzungukwa na scandal kibao kuhusu wanawake, Diamond ni kijana
mwenye mawazo pevu na ya kiutuuzima. Akiwa ametoka kwenye familia duni
na kupata misukosuko mingi ikiwemo kutengwa na baba yake na kulelewa
zaidi na mama yake, Diamond amekuwa akitoa ushauri na kuwapa moyo
watafutaji wa maisha wasikate tamaa. Hupenda kutoa ushauri kwa vijana
wenzie kuhusiana na umuhimu wa kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu
mwenyezi Mungu na kutokata tamaa.
Katika kuhakikisha kuwa anaitolea pia jamii, hivi karibuni alitangaza
kuwa na nia ya kujenga msikiti. Ni kwa sababu zipi kijana huyu asiwe na
ushawishi?
Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza
kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti
yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa
maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na
kampuni ya IPP.
Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa
Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho
Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika,
Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa
vipindi bora kabisa Clouds FM.
Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na
wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa
Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana
zaidi ya followers 40,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes
zaidi ya 90,000.
Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na
kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine
kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku
akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki. Pamoja na
kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu
anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu
wa watu.
Nancy Sumari ni msichana mrembo, mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania
wa kwanza aliyewahi kufika mbali zaidi kwenye shindano la Miss World
ambapo mwaka 2005 alifanikiwa kuwa Miss World Africa.
Kwa sasa Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anasoma Shahada ya Biashara. Pia
ni mjasiriamali na anafanya kazi zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha
watoto wa kike kujitambua na kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao.
Katika harakati zake za kuhakikisha wasichana wa Tanzania wanatambua
haki zao, anaendesha programu iitwayo Mentorship, ambayo inazunguka
kwenye shule mbalimbali za serikali za wasichana nchini, na kuzungumza
nao kuhusu maisha. “Kwenye programu hiyo, tunabadilishana mawazo na
wanafunzi na wao wanazungumza changamoto wanazokutana nazo na kupeana
mawazo jinsi ya kufanya kwani nawaambia wakiamua kuthubutu wanaweza
kufanikiwa, na wanaonesha wanaweza,”Nancy aliliambia gazeti la Habari
Leo hivi karibuni.
Pamoja na hayo pia Nancy anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania
(TEA), kwenye kampeni ya kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za
sekondari za serikali nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata
elimu.
Hivi karibuni alizindua kitabu chake kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’
kinachomlenga mtoto wa kike kuona jinsi wanawake wengine walivyofanikiwa
licha ya kupitia changamoto mbalimbali.
“Ninaamini kitabu kitasomwa na wengi ndio maana nikaamua ujumbe wangu
niufikishe kwa njia hii, watasoma watoto wetu hata wajukuu kitajenga
kitu kwenye akili ya mtoto na wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao
watathubutu” aliliambia Habari Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa
kutoka kwa mrembo huyu
0 maoni:
Chapisha Maoni