Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi la
Tanzania wamefanikisha kuifungua barabara ya Kongowe kuelekea Mjimwema
hadi Kigamboni ambayo ilijifunga kutokana na kukatika kwa kalvati katika
mto Mtokozi . Kalvati hilo lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha kwa
siku kadhaa hapa jijini.
Hapo
jana siku ya Jumanne, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pia
alishirikiana na watendaji kwa siku nzima akiwa eneo la Mpiji
kuhakikisha barabara ya Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo inaanza kupitika
tena baada ya kuwa imejifunga kwa takriban siku tatu. Sehemu hii ya
barabara iliathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha
katika kipindi cha hivi karibuni. Matengenezo katika daraja la Mpiji
yalikamilika jana usiku na magari yameanza kupiti bila ya matatizo.
Siku
ya Jumatatu daraja jingine katika katika mto Kizinga kwenye barabara ya
Kilwa eneo la Mbagala Kongowe ilifunguka baada ya kazi ya usiku kucha
iliyoongwozwa na Waziri Magufuli kufanikisha kukamilisha matengenezo
katika sehemu hiyo yenye magari mengi. Barabara ya Kilwa ndiyo kiungo
kikuu cha usafiri wa barabara kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.
Aidha
katika siku hiyo hiyo ya Jumatatu, daraja la Ruvu pia lilianza kupitisha
bagari baada ya sehemu ya barabara iliyokuwa imeharibika kutokana na
mafuriko, kukarabatiwa.
Matengenezo yakiendelea katika Daraja la Mpiji.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia matengenezo katika Daraja la Mpiji.
Waziri Magufuli akijionea madhara ya mafuriko katika barabara ya Kilwa eneo la mto Mzinga eneo la Mbagala Kongowe.
Waziri Magufuli akiwa kazini usiku katika eneo la mto Kizinga.
Hali ilivyo sasa katika eneo la Mto Kizinga kwa sasa.
Hali ilivyokuwa katika daraja la Mto Mtokozi katika barabara ya Kongowe - Mjimwema - Kigamboni.
Hali ilivyo sasa katika barabara ya Kongowe - Mjimwema - Kigamboni.
0 maoni:
Chapisha Maoni